Monday, August 31, 2015

MPENDAZOE, LEMBELI, KATAMBI WAITEKA SHINYANGA MJINI

Mheshimiwa James Lembeli akimwombea kura mgombea urais wa Ukawa mheshimiwa Edward Lowassa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa wakazi wa Shinyanga


Mgombea ubunge jimbo la Kishapu kupitia Ukawa ndugu Fred Mpendazoe akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watanzania kukubali mabadiliko kwani CCM imechoka huku akisisitiza kuwa mgombea urais wa CCM John Magufuli hana kabila zaidi ya kabila la CCM ambayo kamwe haiwezi kutoa rais bora

Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema pamoja na hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa CCM akiwemo mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo Stephen Masele hatakata tamaa kuwapigania haki wananchi na kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya wananchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uenezi kanda ya ziwa Chadema Juma Protas akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ambapo aliwasisitiza wananchi kuchagua viongozi wa Ukawa ambayo ndiyo mwarobaini wa maendeleo ya watanzania
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Msalala Paul Malaika akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema hata kama kuna mgombea mwenye sifa nzuri ndani ya CCM wananchi wasimchague kutokana na kwamba mfumo mzima wa CCM ni mbovu hivyo wafanye mabadiliko kwa kuiweka Ukawa madarakani
Mheshimiwa James Lembeli na fimbo yake ya kimila akimsikiliza kwa umakini zaidi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la Shinyanga
Makamanda wa Ukawa wakiwa meza kuu
Wagombea udiwani kupitia Ukawa katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga wakitambulishwa wakati wa mkutano huo
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano


1 comment: