Sunday, August 9, 2015

Mgombea Urais na Mgombea Mwenza Kupitia CHADEMA na UKAWA ndugu Edward Lowassa na Ndugu Juma Duni Hajji kuchukua Fomu ya kuteuliwa Kugombea Urais kwenye ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku ya Jumatatu Tarehe 10 Agosti 2015

Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA unapenda kuwatangazia watanzania wote kuwa Tarehe 10/8/2015 Mgombe urais kupitia CHADEMA na UKAWA Edward Lowassa na mgombea mwenza Juma Haji Duni watachukua fomu ya kugombea urais kwenye ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Makutano yataanza Makao makuu ya CUF Ilala saa 3 asubuhi kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kumalizia Makao Makuu ya CHADEMA kinondoni.
Akiongea na waandishi wa habari kwa kuwawakilisha makatibu wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA (katikati) ni Salum Mwalim aliyekaimu nafasi ya katibu mkuu CHADEMA (kulia kwake)Frorian R Mbeo mwakilishi wa katibu Mkuu wa NCCR (kushoto kwake)Tozzi Matwanga katibu mkuu NLD
Tunawaomba watanzania wapenda mabadiliko kujitokeza kwa wingi


No comments:

Post a Comment