Sunday, August 16, 2015

MAELFU YA WAKAZI WA MWANZA WAMLAKI MH EDWARD LOWASSA

Mgombea urais wa UKAWA Mh. Edward Lowassa ameendelea na ziara yake ya kutafuta wadhani ambapo alianzia jijini Mbeya tarehe 14/8/2015 katika viwanja vya Rwanda nzovwe maarufu kama uwanja wa Dr Slaa na kufuatiwa Jijini Arusha tarehe 15/8/2015 katika viwanja vya Tindigani na kumaliziwa Jijini Mwanza tarehe 16/8/2015 katika viwanja vya Furahisha. Katika mikutano yote hiyo kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea urais wa UKAWA. Alipotua katika kiwanja cha ndege Mwanza alikutana na umati mkubwa wa watu waliomsindikiza mpaka sehemu ya tukio.
Mbali na kuwa na umati mkubwa wa wafuasi katika mikutano hiyo viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wameendelea kusistiza kuwa Watanzania wajitokeza kwa wingi wao siku ya kupiga kura na walinde kura zao na huku wakitoa matamko mbalimbali juu ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kusimamia haki na kulinda usalama wa Watanzania sio kutumika na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi na kuwa hali hiyo ikipuuzwa italeta machafuko katika Taifa.


No comments:

Post a Comment