TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
15 Julai 2015
CUF NA UKAWA
Waheshimiwa waandishi wa Habari
Chama cha wananchi CUF tukiwa sehemu ya UKAWA tunaendelea na vikao vya kuafikiana na maamuzi kwa hoja mbalimbali zinazohusu uimarishaji wa malengo ya uanzishwaji wa UKAWA.
Katika kikao cha UKAWA kilichofanyika tarehe 14 Julai 2015 Collesium Hotel Dar es Salaam, CUF hatukuweza kushiriki kikao hicho.
Sababu za kutoshiriki kwetu katika kikao hicho, kumetokana na sababu za kikatiba za ndani ya CUF kwa kuwa katika maamuzi yote yanayohusu masuala mazito ya kinchi kama haya,tuna desturi ya kukaa na kujadiliana kama chama kwanza katika kuafikiana na jambo lolote lile muhimu kwa maslahi ya taifa kama vyama vingine vinavyofanya.
Baada ya kikao cha UKAWA cha 11/07/2015 CUF tume kuwa na vikao vinavyohusisha viongozi wakuu wa chama yaani Mwenyekiti,Naibu Katibu Mkuu na wakurugenzi na jana tumeendelea na kikao.
Na ndio maana katika kikao cha UKAWA Mwenyekiti Prof.Lipumba na sisi viongozi wa kuu hatukuweza kuhudhuria.
Kutohudhuria kwa kikao cha tarehe 14 Julai 2015, hakuna mahusiano yoyote na uvumi kwamba CUF imesusia au kujitoa katika UKAWA kama baadhi ya mitandao ya kijamii au vyombo vya habari vilivyoripoti pamoja na maneno ya chini kwa chini yanayoendelea kwa wananchi, bali ni kutokana na baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la taifa kutoka mikoani na wanachama wetu maeneo mengi ya nchi kuutaka uongozi wa Chama kusitisha kwa muda kuhitimisha maamuzi ya kumpata mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupeperusha bendera ya UKAWA mpaka kuwepo kwa ridhaa ya Chombo hicho cha kikatiba.
Aidha Chama kinatambua kwamba hivi sasa tumebakiwa na muda mfupi kabla ya kuingia katika mchakato rasmi wa kuchukua fomu za serikali kuomba kuteuliwa kuwania uongozi, hivyo Chama kimeitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la taifa hapo tarehe 25 Julai 2015 ilikupata Baraka ya chombo cha maamuzi kama ambavyo wenzetu washirika wa UKAWA wamekwishapitia hatua hizi katika vyama vyao.
Watanzania watambue kwamba Nchi inapitia katika kipindi kigumu sana, ongezeko la majimbo 26 ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi,kwa kipindi cha chini ya siku 45 kabla ya kuanza kampeni ni changamoto ambazo UKAWA tunapaswa kuyafanyia kazi ili kuona namna gani tunajipanga kwa mazingira haya.
CUF tuanaamini kwamba kwa maridhiano ya pamoja ndani ya vyama vyetu na ndani ya UKAWA tutajenga UKAWA imara na hatimaye kuwa na mgombea mmoja wa Urais,Wabungena madiwani wa UKAWA na hivyo kuiangusha CCM kwenye uchaguzi wa Oktoba 25.
HAKI SAWA KWA WOTE
Magdalena Sakaya
Naibu Katibu Mkuu, Bara.
No comments:
Post a Comment