Katika mgawanyo huo, Jijini Dar es Salaam ni majimbo mawili pekee ndio yaliyoguswa. Majimbo hayo ni Jimbo la Mbagala lililomegwa kutoka Jimbo la Kigamboni na Jimbo la Kibamba lililokuwa sehemu ya Jimbo la Ubungo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ametaja majimbo mengine kuwa ni Jimbo la Handeni katika Halmashauri Mji wa Handeni (Tanga), Nanyamba katika Halmashauri ya Mji Nanyamba (Mtwara), Makambako Halmashauri ya Mji Makambako (Njombe), Bitiama Halmashauri ya Wilaya Butiama (Mara), Tarime mjini Halmashauri ya Mji Tarime (Mara).
Lubuva alitaja majimbo mengine kuwa ni Tunduma lililopo katika Halmashauri ya Mji Tunduma (Mbeya), Jimbo la Nsimbo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo (Katavi), Kavuu Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe (Katavi), Geita mjini Halmashauri ya mjini Geita (Geita), Mafinga mjini Halmashauri ya Mji Mafinga (Njombe).
Majimbo mengine ni Kahama mjini Halmashauri ya Mji Kahama (Shinyanga), Ushetu kwenye Halmashauri ya Wilaya Ushetu (Shinyanga), Nzega mjini lililopo kwenye Halmashauri ya Mji wa Nzega (Tabora), Kondoa mjini Halmashauri ya Mji Kondoa (Dodoma).
Mengine ni Newala mjini Halmashauri ya mji Newela (Mtwara), Mbulu mjini Halmashauri ya Mji Mbulu (Arusha), Bunda mji Halmashauri ya mji Bunda (Mara), Ndanda Halmashauri ya Wilaya ya Masasi (Mtwara), Vwawa Halmashauri ya Wilaya Mbozi (Mbeya), Manonga Halmashauri ya Wilaya Igunga (Tabora).
Majimbo mengine ni Mlimba Halmashauri Kilombero (Morogoro), Madaba Halmashauri ya Wilaya Madaba (Ruvuma), Ulyankulu Halmashauri ya Wilaya Kaliua (Tabora) na Mbinga mjini Halmashauri ya Mji Mbinga (Ruvuma).
Pia, ameyataja majimbo 10 ambayo yaliyobadilishwa majina majina kuwa, Jimbo la Rugwe Mashariki (Mbeya) na kuwa Jimbo la Busekelo, Jimbo la Rugwe Magharibi (Mbeya) na kuwa Jimbo la Rugwe, Jimbo la Urambo Mashariki (Tabora) litaotwa Jimbo la Urambo.
Mengine ni Jimbo la Urambo Magharibi (Tabora) na kuwa Jimbo la Kaliua, Jimbo la Njombe Mgharibi (Njombe) na kuwa Jimbo la Wanging’ombe, Jimbo la Njombe Kusini (Njombe) kwamba litaitwa Jimbo la Lupembe.
Jimbo la Bariadi (Simiyu) litaitwa Jimbo la Itilima, Jimbo la Bariadi Magharibi (Simiyu) linakuwa Jimbo la Bariadi, Jimbo la Kondoa Kusini (Dodoma) kuwa Jimbo la Chemba.
Lubuva amesema, ugawaji wa majimbo hayo ulizingatia vigezo muhimu vitatu ambavyo ni wastani wa idadi ya watu, mipaka ya kiutawala na uwezo wa ukumbi wa Bunge.
Amesema, kabla ya kuyagawa majimbo hayo na kuanzisha majimbo mapya tume ilitembelea majimbo yote yaliyokidhi vigezo nakustahili kugawanywa ambapo tume ilikutana na wadau.
No comments:
Post a Comment