Friday, May 8, 2015

Chadema yavamia Majimbo na Kata za CCM Morogoro.

Na Bryceson Mathias, Morogoro.
WATIA Nia wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wamevamia Majimbo na Kata zinazoshikiliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kiasi cha kuwaweka Roho juu wanaokalia Viti hivyo, wakihofu kwamba, mwaka huu wa Uchaguzi watapoteza nafasi zao.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Samwel Kitwika, amesema, Majimbo yote 10 ya Morogoro, yamevamiwa na Watia Nia ya Kugombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema.

Mbali ya Majimbo 10 kuvamiwa, Kitwika amesema, Kata 212 za Morogoro, nazo ziko kwenye Mtikisiko, ambapo wanaowania Udiwani wa Kata hizo, Wanashambulia kwa Mikutano ya hadhara kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi, ili wakati ukifika; Waungwe Mkono.

Kitwika alibainisha idadi ya Watia Nia wa Chadema na jinsia yao kwenye mabano kuwa, “Jimbo la Kilombero lina Watahini 11, Me(9), Ke(2), Mikumi Wanne (Me), Kilosa Kati Watano(Me), Gairo Watatu(Me), Mvomero Wanne(Me), Manispaa ya Morogoro Saba, Me(6), Ke(1),

“Morogoro Kusini Mashariki –Watatu, Me(2), Ke(1), Ulanga Magharibi-Saba, Me(6), Ke(1) na Ulanga Mashariki-Wawili, Me(1), Ke(1), Ulanga Magharibi tuna asilimia 100%, tutashinda.alisema Kitwika.

Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kihonda Maghorofani’A’, Elizeus Rwegasira, baada ya kuibwaga CCM mahakamani Morogoro, sasa ametia Nia ya kuutaka Udiwani wa Kata hiyo, ili apambana na Diwani, anayeshikilia Kata hiyo, Lyidia Mbiaji (CCM,) aliyeapa atashinda.

Aidha Kati ya Wachungaji wawili wanaowania kupitishwa na Chadema kugombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama hicho, James Samson Mabula, alimaarufu Power Mabula, wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT), alikiri kuwa yumo kwenye Kinyang’anyiro cha kuwania kukubaliwa kugombea Ubunge wa Manispaa ya Morogoro.

No comments:

Post a Comment