Friday, April 24, 2015

Chadema yaibwaga tena CCM mahakamani.

Elizeus Rwegasira 

Na Bryceson Mathias, Morogoro.
PAMOJA na hila zinazotengenezwa kuhujumu ushindi wake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa mara nyingine kimekibwaga na kukikanyaga Chama cha Mapinduzi (CCM), na kuibuka na Ushindi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kihonda Maghorofani, uliopingwa mahakamani.

Katika Kesi ya Uchaguzi Na2/2015 iliyofunguliwa na, Waziri Makumlo [CCM] dhidi ya Kamanda, Elizeus Rwegasira Tiilaga [CHADEMA], Kesi hiyo imefutwa na Rwegasira (Chadema), kupewa Ushindi wa kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kihonda Maghorofani.

Makumulo [CCM] ambaye aliyeongozwa na Msomi (Wakili), Tumaini Mfinanga, alionesha kukata tamaa ya kupata Ushindi kutokana na kutoonekana mahakamani kuendelea na Kesi, dhidi ya Rwegasira aliyetetewa na Msomi (Wakili) Mahili, Barthromeo Tarimo (Chadema).

Kutokana na mlalamikaji [Makumlo] kutohudhuria kwenye kesi mahakamani hapo mara mbili (2) mfululizo, Makumulo alisababisha kukosa mawasiliano na Wakili wake Msomi Mfinanga, ili wapambane kisheria na Msomi mwenzake (Tarimo).

Makumulo kutotokea mahakamani, kulipelekea Wakili wa Mlalamikiwa (Rwegasira), Msomi Tarimo, kuiomba Mahakama, Shauri hilo lifutwe, jambo lililoungwa mkono na Mwakilishi wa Manispaa pamoja na Wakili wa mlalamikaji [Mfinanga].

Mbali ya kutooneka, Makumulo alipigiwa simu na Wakili wake siku ya kesi bila kupokea; na kwa hali hiyo; Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro Agnes Ringo, aliifuta Kesi hiyo na Kumtangaza Rwegasira (Chadema), kuwa Mshindi wa Uchaguzi huo, baada ya kusubiriwa kwa Nusu Saa bila kutokea.

Ushindi wa Rwegasira, unakuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia, kutangaza majina ya Wakurugenzi watano waliosimamishwa kazi na wengine sita waliopewa onyo kutokana na uchunguzi kuonyesha walishindwa kutekeleza wajibu wao kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tareheDesemba 14, lMwaka jana.

No comments:

Post a Comment