Monday, April 27, 2015

Benedicto Mtungirehi aachana rasmi na TLP na kujiunga na CHADEMA

Hatimaye aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kyerwa kupitia TLP mwaka 2000-2005 na baadaye kuangushwa kwa mizengwe katika uchaguzi mkuu wa 2005 amerejea ulingoni kwa kujiunga na makamanda wa CHADEMA leo katika makao mkuu ya wilaya mpya ya Kyerwa huko Kaisho.
Itakumbukwa katika kipindi cha ubunge wake ni kati ya wabunge waliokuwa machachari na walioinyima usingizi serikali kipindi hicho akiwa na kina Slaa na Rwakatare wa Bukoba Mjini.
CCM ndio mwisho kwa ukanda huo ikizingatiwa ilishazikwa katika serikali za mitaa katika jimbo la Karagwe.
Chanzo watu walio karibu na Mtungirehi pamoja na katibu mwenezi CHADEMA, mpaka sasa waliotia nia kugombea ubunge jimboni humo wamefikia 12.

No comments:

Post a Comment