Friday, April 17, 2015

BAVICHA Watikisa Majiji Matatu Tanzania

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA ) Wamezidi kudhihirisha umahiri wao katika,kuhakikisha wanaipoteza na kuifuta Ccm katika medani za siasa ya Tanzania.

BAVICHA wamefanya mashambulizi makali katika Jiji la Mbeya,Mwanza na Musoma.Kama ambavyo,lengo kuu la BAVICHA nikuona CHADEMA kwa kushirikiana na UKAWA wanakwenda Ikulu mwaka huu, wa uchaguzi 2015 wameamua kutumia fursa hii kuendelea kuisambaratisha Ccm kila kona ya nchi hii.

Mashambulizi haya yameendelea kuongozwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa PATROBAS KATAMBI,ambae yeye alikuwa Mwanza kwaajili ya kuhakikisha matawi ya CHASO yanafunguliwa katika CHUO CHA MIPANGO Mwanza,jambo ambalo limefanikiwa na kuzaa matunda makubwa kwani alifanikiwa kuvuna wanachama wapya miatatu kutoka CCM.

Huku katika Mji wa Musoma...,Katibu Mkuu wa BAVICHA Julius MWITA aliwashamoto,na kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika kumsikiliza na kumshangilia kwa kila hoja aliyokuwa akiizungumzia kwakuwa alisema kweli tupu.

Katibu Mkuu huyo hakusita kugusia swala la ukosefu wa ajira kwa vijana na jinsi Serikali ya CCM ilivyoshindwa kuzalisha ajira kwa vijana,badala yake wasomi wanaomaliza vyuo vikuu wapo mtaani hawana kazi za kufanya.

Julius Mwita...,alihoji juu ya Upungufu mkubwa wa Askari katika vituo vya Polisi jambo ambalo,haliingii akilini wakati vijana wapo mitaani wamemaliza Sekondari na Vyuo hawana ajira.

Huko nako katika Jiji la Mbeya...,M/kiti wa Mkoa wa BAVICHA George Tito amezidi kutishia uhai wa Ccm katika Jiji hilo,baada ya kufanya ziara vijijini ilikuimarisha Chama upande huo.Akiwa katika Kata ya Ushirika alipokelewa kwa Maandamano makubwa na vijana waliokuwa wakimsubiri kwa hamu tokea saa1 Asubuhi.

Akizungumza katika mkutano huo George Tito,aliweka wazi jinsi Serikali ya Ccm imewasahau wananchi wanaoishi vijijini,nakuwaona hawanathamani mara baada ya kuiweka madarakani.

"Serikali ya Ccm imeshindwa kuona thamani yenu,wana wa Ushirika imewasahu na kuona hamna maana tena.Sasa uchaguzi umefika watarudi tena kwenu kuomba kura kama walivyokuja mwaka 2010, mka wapa kura zenu sasa wanakuja kwa style ilele ya Vilemba,Kapelo,Kanga na Tirshet kuwahonga tafadhali msikubali hata kidogo.


No comments:

Post a Comment