na Bryceson Mathias, Hale-Tanga.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemuonya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe, Lukasi Mweri, aache kufanya Shughuli za Siasa akikibeba Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwa madai Jamii ikichoshwa, ataibua Maaafa.
Akizungumza katika Kampeni za Uchaguzi Desemba 8, mwaka huu, Miji ya Mnyuzi na Hale Mwakinyumbi Korogwe, Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Aulelian Nziku, amemuonya Mweri asifanye Siasa kuihujumu Chadema na kuibeba CCM.
“Chadema tunamuonya Mweri na DAS Korogwe, Stanley Madyaga, waache Siasa Chafu za kuihujumu Chadema kwa Mapingamizi Batili yanayowekwa na CMM, badala yake watenda Haki kwa Mujibu wa Kanuni na sheria, la sivyo Jamii ikichoka lolote likitokea, Watawajibika.
Uhalali wa Mihuri ya Chama cha Chadema, ambayo imewekewa Pingamizi kwa Wagombea wa Wenyeviti ndiyo hiyo hiyo ambayo imetumika kwenye Fomu za Wagombea wa Ujumbe, lakini hao hawakuwekewa pingamiza ila Wenyeviti, Kulikoni? ”.alisema Nziku
Aidha Nziku alisema, Chama wilayani humo kwa kushirikiana na Chadema Mkoa wa Tanga, kinafanya Mawasilino na Chadema Taifa ili kupata Ushauri wa kuwapeleka Mkurugenzi Mweri na DAS Madyaga, mahakani, ili kupinga kuwafuta na kuwaondoa Wagombea wa Chama chake.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi, Mweri, alikanusha Tuhuma za kuibeba CCM akidai, “Kwa Kanuni Mimi ni Msimamizi wa Uchaguzi, sihusiki na Maamuzi ya Mapingamizi, ila Kamati inayoongozwa na DAS Madyaga”.alisema Mweri.
Mwandishi alipomtafura DAS wa Korogwe Madyaga katika simu Simu yake, 0713300223, lakini simu yake iliitaa bila majibu, na alipoandikiwa ujumbe mfupi, hadi tunakwenda mitamboni, hakutoa jibu lolote kuhusu malalamiko ya maamuzi Kamati yake ya kukibeba CCM.
No comments:
Post a Comment