MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mtaa wa Kikombo Makulu, Eliakimu Kutusha amesema, Chama chake kitaibuka Mshindi na kuzoa Viti vyote vya Kata ya Kikombo kwenye Uchaguzi wa SAerikali za Mitaa.
Akizungumza baada ya kushinda kura ya Maoni ya Chadema Novemba 7, mwaka huu, Kutusha alisema, hakuna Ubishi Chadema Kata ya Kikomo, kitazoa viti vyote vya Serikali za Mitaa kwa sababu Chama chake kina wagombea wazuri wanaokubalika na kimejipanga.
Kutusha alipuuza majigambo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema, “Majigambo hayo ni kama ya Nyani Mtoto aliyechekelea Msitu unapoungua, huku akiwa hajui utakapoungua usiku atakuwa hana Nyumba kulala”
Wajumbe wa Chadema walioshinda katika Kura hiyo ya maoni katika Mtaa wa Makulu na ambao watachuana na wale wa CCM ni pamoja na, Amosi Matata, Yohana Ndahani, Elia Nyagani, Aidani Mbavu, Roy Mbalayi, na Pendo Mazengo.
Wananchi waliohojiwa baada ya kura hiyo ya maoni, wengi wamesema, Kikosi hicho cha Washindi ni Kikali kwa sababu ndicho kilichowezesha kumng’oa mmoja wa watendaji Kata na Polisi wa Kata, waliokuwa Mzigo katika Kata hiyo.
Mitaa ya Kata ya Kikombo ambayo iko kwenye kinyang’anyiro hicho ni Mitatu ambapo, imetajwa kuwa ni pamoja na Kikombo Makulu, Kikombo Mnandani, ambapo Mgombea wake ni, Ilumbo Ndaga, na Mtaa wa Kikombo Chololo, ambapo washindi watajulikana kesho.
Naye Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kikombo Chadema anayetarajiwa kugombea kiti hicho akiridhiwa na Chama chake, Yona Kusaja, amedai, kama atakuwa na Kikosi kilichopitishwa katika kura hiyo ya maoni, Ushindi wa Udiwani kwake Kikombo, ni kama Maji ya Kunywa.
No comments:
Post a Comment