Wednesday, November 12, 2014

KATIBU WA CHADEMA DMV, MAREKANI, ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CHADEMA TANZANIA



Katibu wa tawi la CHADEMA DMV, Marekani, Ndugu Liberatus Mwang'ombe amefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya CHADEMA jijini Dar Es Salaam.

Katika ziara hiyo Ndugu Liberatus Mwang'ombe aliweza kufanya mkutano na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa na mratibu wa mambo ya wabunge  wa CHADEMA, Ndugu John Mrema.

Ndg. Liberatus Mwang'ombe alipata fursa ya  kujadiliana mambo mbalimbali na Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa Dr Wilbroad Slaa hosusani changamoto zinazo wakabili Watanzania kwa ujumla na mbinu za kukabiliana nazo.

Zaidi walijadili namna ya kutatua changamoto hizo na kuhakikisha Tanzania inakuwa ya Watanzania na sio watu wachache.



No comments:

Post a Comment