Saturday, September 20, 2014

CHADEMA haitaangamizwa na Watu Waovu.

Na Bryceson Mathias, Morogoro.
BAADA ya kukamilishwa kwa Chaguzi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) toka Ngazi ya Msingi hadi Taifa, mbali ya kuupongeza Ucgaguzi huo, Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Mhonda Magorofani , Elizeus Rwegasira, amesema, Chadema haitaangamizwa na Watu na Waovu.

Akizungumzia misukosuko inayopitia Chadema na Viongozi wake ikiwemo kukwamishwa na Vyombo vya Usalama, Jeshi la Polisi, Chama Mapinduzi (CCM) na Waasi wa Chama hicho katika harakati zake, ambapo Rwegasira alimnukuu Falsafa za Bill Gates na Albert Einstein.

“Albert Einstein alisema, ‘Dunia haitaangamizwa na watu wanaotenda maovu, isipokuwa itaangamizwa na wale wanaoangalia uovu ukitendeka na hawachukui jitihada za kuuzuia.

“Bill Gates alisema, ‘Watu mara zote wanaogopa mabadiliko kutokana na ujinga na ujinga huo ndio unaowafanya watu kuwa na hofu kuu”.alisema Rwegasira.

Rwegasira alisema maneno hayo ya uwajibikaji, baada ya Uongozi wa Chadema Kata ya Kihonda Magorofani, kuridhia na kupongeza Hotuba zote za Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alizotoa katika chaguzi za, BAVICHA, BAWACHA na Uchaguzi wa Taifa uliomrejesha kuwa Mwenyekiti.

Alisema, Safu ya Uongozi wa Kata hiyo, Mwenyekiti, Elizeus Rwegasira, Katibu, Mbaraka Haji, Katibu mwenezi, Linti Linti, Mwekahazina, Elizabeth Magambo, Mwenyekiti wa wazee, Fanuel Muya, upo tayari kutekeleza Maagizo ya Chadema Taifa kama yalivyoelekeza..

Wengine katika uongozi huo ni, Katibu wa wazee, Engilbert Kihwili, Mwenyekiti wa wanawake, Doroth Kweka, Katibu wa wanawake, Elizabeth Magambo. Mwenyekiti wa Vijana, Issa Kipanje, Katibu wa Vijana, Revocatus Rugakingira, na Mwakilishi wa Jimbo, Asifiwe Mkumbo.

Rwegasira alidai, 27/9/2014 watakuwa na Semina ya viongozi wa kata, matawi na misingi juu ya majukumu yao, na Mwezi wa Oktoba na kuendelea mwaka huu, Kila mwezi watakuwa na mikutano miwili ya hadhara kuhusu, Falsafa, Dira, Sera za Chadema na kero za wananchi.

Alisema CHADEMA kinaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi waliochaguliwa wajitwalie mamalaka ya Umma na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

Aliongeza kwa kusema, Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.

No comments:

Post a Comment