Sunday, August 31, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (TCD) IKULU NDOGO DODOMA LEO

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo , Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Isack Cheyo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mhe Fahmi Dovutwa wakielekea chumba cha mikutano Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo 

Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo





Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo



No comments:

Post a Comment