Saturday, July 19, 2014

TAARIFA FUPI KWA VYOMBO VYA HABARI

Kutokana na masuala mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya chama, ambayo wanachama na Watanzania kwa ujumla wanahitaji kusikia kauli, msimamo na maelekezo ya chama, CHADEMA inatarajia kukutana na waandishi wa habari siku ya Jumanne, tarehe 15 Julai, 2014.
Kupitia press conference hiyo itakayofanyika Makao Makuu, Kinondoni Dar es Salaam, kama ilivyo ada chama kitazungumza masuala ya msingi yanayohusu maslahi na matakwa ya wanachama na Watanzania.
Vyombo vya habari vyote vimealikwa kuhudhuria mkutano huo, unaotarajiwa kuanza saa 5.00 asubuhi.
Pamoja na kuvialika vombo vya habari ambavyo vitauhabarisha umma mkubwa wa Watanzania juu ya kitakachojiri kesho, tunapenda pia kupitia njia nyingine za utoaji taarifa rasmi za chama, (www.chadema.or.tz, chademataifa (twitter account), Kurugenzi ya Habari (Facebook), Kurugenzi ya Habari (Jamii Forums & Mwanahalisi Forums Account), tunapenda kuufahamisha umma juu ya press conference hiyo ya kesho.

Imetolewa leo Jumanne, Julai 14, 2014 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari- CHADEMA

No comments:

Post a Comment