Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana jijini Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia Ijumaa ya tarehe 18-19 Julai, 2014, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika siku mbili hizo, wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA watajadili pamoja na masuala mengine;
· Mchakato wa Katiba Mpya.
· Taarifa ya hali ya siasa nchini.
· Uchaguzi wa ndani ya chama.
· Taarifa ya fedha, Mpango Kazi na Bajeti.
· Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba, Kanuni na Miongozo ya Mabaraza ya Chama.
· Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
· Taarifa ya Katibu wa Wabunge.
· Rufaa mbalimbali.
· Nembo na Kadi za Mabaraza ya Chama.
Kikao hicho kitatanguliwa na hotuba ya ufunguzi ambapo vyombo vya habari vinaalikwa kuhudhuria.
Imetolewa leo Alhamis, tarehe 17 Julai, 2014 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari- CHADEMA
No comments:
Post a Comment