Tuesday, April 1, 2014

CCM yadaiwa kutishia Ajira za Walimu wanaoiamini Chadema!

Na Bryceson Mathias, Morogoro.

VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Morogoro, wanatuhumiwa kuwatishia Walimu wanaoonekana ni Wafuasi wa Chama cha CHADEMA, ambapo miongozi mwa Walimu wenye Vyeo, wanadaiwa kutumika kuwafuatafuata katika maeneo yao ya kazi, ili Ajira zao zisitishwe.

Hayo yamebainika katika Makundi ya Viongozi wa CCM wa Wilaya mkoani Morogoro, waliomdokeza Mwandishi wetu kwamba, kutokana na Walimu hao kutishia uwepo wa baadhi ya Wabunge katika Majimbo yao mwaka 2015, Wameamua kuwatishia Nyau Walimu hao.

Walimu Wanne wa Wilaya za Mvomero, Kilosa, Gairo na Kongwa inasemekana tayari wameonja Joto hiyo ya Jiwe, ambapo mmoja wao ameapa akisema, Iwapo wana siasa Uchwara na Mbunge mmoja anayekataliwa na wananchi  atathubutu kumfuata, atamburuza mahakamani.

“Ni kweli mimi ni mmoja wa ambao nimeandikiwa barua na Mwalimu wangu Mkuu Msaidizi, kwamba nimekuwa nikionekana kwenye mikutano ya Chadema, hivyo natakiwa nijieleze kwa maandishi, ili nisichukuliwe hatua za kinidhamu.

“Binafsi sina Mashaka, kwa sababu najua hakuna Mzazi anayeweza kumchagulia Mwanae Mume au Mke wa kuishi naye isipokuwa wenzi wenyewe, hivyo nangojea tishio hilo la Nyau linifikie ili name nitoe majibu”.alisema Mwalimu huyo aliyeomba asitajwe jina lake.

Walimu hao walisema, wanataka kuunganisha Nguvu kuweka Mawakili Sita makini nchini watakaowatetea kwa umoja wao, pindi ujinga huo utakapoibuliwa na kuwa Kesi, ili warumbane kisheria mahakamani, kama ipo Sheria ya kumlazimisha mtu kupenda Chama asichokitaka.

Aidha mmoja wa wanasheria maarufu wa kujitegemea mkoani Morogoro ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema, “Hakuna Sheria inayomlazimisha mtu kupenda kitu asichokipenda, hivyo kitendo kinachofanywa na wanasiasa hao kinakiuka hakiza Binadamu kwa faida yake.

No comments:

Post a Comment