Sunday, March 9, 2014

Wapenzi Chadema wadai kubaini hujuma za Green Guard-Kilombero.

na Bryceson Mathias,

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Kibaoni wilayani Kilombero, kimedai kubaini Tuhuma na Njama zinazofanywa na Vijana wa ‘Green Guard’ wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, wanaokusudia kukihujumu Chama hicho katika Uchaguzi ujao wa Diwani wa Kata hiyo.
Chadema kilidai kubaini Njama hizo kufuatia Wananchi wa Kata, kumtupia Lawama Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Azimina Mbilinyi na Serikali Kuu, kutoiodhesha Kata yao katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani wa Kata 27 uliofanyika karibuni, hali wakijua hawana Diwani.kwa miezi Tisa sasa.
Tanzania Daima ilimpigia bila kujibiwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Mbilinyi Simu 0786 091342 ili aelezee kwa nini Kata hiyo haikuorodheshwa katika Kata 27 zilizofanya Uchaguzi 16.2.2014, wakati ilikuwa na sifa za kuwemo, kutokana na aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kufariki tangu Mei 29, 2013.
Gazeti halikuishia hapo lilimtafuta Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kibaoni, Odrick Matimbwi, na kukiri Interejensia ya Chama chao kupata taarifa hizo toka kwa wapenzi na Wananchi kuhusu kuwepo kwa taarifa za njama za kundi hilo kuchukua mafunzo ya kukihujumu, lakini akasema Chadema hakitapuuzia, itachukua hatua.
Aidha alisema, Ofisi yake ya Kata na Hata Ofisi ya Chadema Wilaya, kwa pamoja zimechukua hatua ya kuulizia uongozi wa wilaya na Mkurugenzi Mbilinyi dhidi ya kucheleweshwa kwa Uchaguzi huo, lakini hakuna majibu ya maana yanayotolewa na wananchi wanaendlea kukosa mwakilishi wa kuwatumikia.
Kiti cha Diwani wa Kata ya Kibaoni kipo wazi kwa miezi tisa sasa tkufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Salum Msika, huku wachumi na wadau wa mambo ya maendeleo wakilalamikia kwamba, Shughuli za Maendeleo ndani ya Kata kudorola kwa kukosa Diwani wa kuzisukuma kwa ukaribu zaidi.
Hata hivyo katika majibu ya upande wa wadau wa siasa wilayani Kilombero na wananchi wa Kata hiyo, wamelitonya Tanzania Daima wakidai kwamba, Viongozi wa Serikali na wale wa Wilaya, huenda wanahofia hali tete ya upepo wa kisiasa, ambapo upinzani upo juu zaidi katika eneo hilo..

No comments:

Post a Comment