Tuesday, February 25, 2014

Dk. Slaa: Nimekuja kuwapa mbunge

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka wananchi wa Jimbo la Kalenga mkoani hapa kutambua kuwa chama hicho kipo kwa lengo la kuwatetea wananchi bila kujali itikadi za vyama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ifunda, Dk. Slaa alilitaka jeshi la Polisi kutenda haki kwa vyama vyote kutokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo ya wapinzani pale wanaposhambuliwa.
Alisema Jeshi la Polisi lisitumie kauli hiyo kuwanyanyasa wapinzani.
Aliwata wananchi wa Ifunda kutambua mbunge wanayemuhitaji awe na vigezo vya kujenga hoja za kuwatetea na kuwaletea maendeleo.
Wakati huo huo, Chifu wa kabila la Wahehe, Abdu Sapi Mkwawa, amevitaka vyama vilivyosimamisha wagombea Kalenga kuendesha kampeni zao kwa amani na utulivu, na akatoa baraka zake kwa mgombea wa CHADEMA na kumtakia ushindi katika Jimbo la Kalenga.

No comments:

Post a Comment