KATIKA hali inayoonesha Umakini wa Chama cha Chadema kusimamia maamuzi yake ya kuachana na ajenda za Wasaliti ili kisitoke kwenye hoja muhimu, sasa kimejikita kwenye mikakati mizito ya 2014, ambapo jana wanachama 35 wa Chama Tawala (CCM) wamejiunga na CHADEMA.
Wanachama hao wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni wale wa Kijiji cha Kisala wilayani Mvomero, ambao katika Kijiji chao Ng’ombe zaidi ya 15 walikatwa miguu ya mbele na ya nyuma na kuwa Vibutu kutokana na vurugu za wakulima na wafugaji.
Wakizungumza katika mkutano huo, Mgombea Udiwani wa Kata ya Sungaji 2010, Jairos Msigwa, aliwataka wananchi waachane na Propaganda za CCM na kujiunga na CHADEMA akidai kwamba,
“Wakati CCM kimeacha kushughulikia Sera Mbovu ya Wakulima na Wafugaji na badala yake kueneza Usaliti ndani ya Chadema, chadema kimejikita kutatua kero zenu na maazimio ya ajenda sita za chama, ikiwa ni pamoja na bei ya Umeme iliyoanza kuwaumiza na Katiba”.alisema Msigwa.
Diwani wa Viti Maalum (Chadema), Juliana Petro, aliwataka akina mama kuondokana na woga wa kudai haki zao, alikumbusha kuna ujanja ujanja wa viongozi kuhusu kero ya Daraja la Kisala akidai hakuna fedha iliyotengwa na hadi leo wanateseka licha kuambiwa kila siku.
Aidha Diwani wa Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, aliwashauri wananchi, kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu (2014), waondokane na Viongozi wababishaji wasiokuwa na dhamira kuwasaidia, na badala wawachague viongozi makini wa chama chake, ambao watalinda haki zao.
Wakaribie ila wasije kuwa wasaliti hapo baadae kama ZZK
ReplyDeletePeoples? Peoples? Power......
ReplyDelete