Saturday, January 18, 2014

Wamuunga Mkono Silinde, DC na DED Watimuliwe.

WANANCHI wa Kata ya Sungaji na Hembeti waliofiwa na Ndugu na kuwa na Walemavu wa kudumu kwa ajili ya Mapigano ya Wakulima na Wafugaji Mvomero, wameunga Mkono hatua ya Mbunge wa Mbozi Magharibi, David  Silinde, kutaka Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Kiteto wafukuzwe Kazi.

Silinde ambaye ni Waziri Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Katika Taarifa yake kwa Vyombo vya Habari kuhusuMgogoro wa Ardhi Kiteto; amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amshauri Rais awafukuze kazi Mkuu wa Wilaya  na Mkurugenzi wake. 

WANANCHI wa Mvomero waliohojiwa kwa nyakati tofauti, wamempongeza Silinde kutumia nafasi ya Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), wakiunga Mkono  watendaji hao watimuliwe baada ya kupata taarifa za kina , na ikibidi aitaarifu na kuishauri Kambi ya Upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA,  ichukue hatua za kibunge  nje na ndani.

Walishauri, ni kweli lipo tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi nchini, hivyo Mbunge huyo na kambi yake ifike katika maeneo yaliyoathirika ili iongee na waathika hao na  kupata picha halisi ilyojiri kwa wananchi hao kwa nchi nzima ili izitendee kazi kero hizo.

Katika Taarifa yake ya Januari 16, 2014 katika Mitandao ya Kijamii, Silinde alimtaka Waziri Mkuu, Pinda, amshauri Rais Jakaya Kikwete awafukuze kazi Mkuu wa Wilaya, Martha Umbulla, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Jane Mutagurwa . 

“Kutokana na mgogoro mkubwa wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji unaoendelea wilayani Kiteto ambao umefikia hatua ya kusababisha maafa makubwa ya umwagikaji damu, mauaji ya watu na uharibifu wa mali, Wizara Kivuli, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), inatoa taarifa ifuatayo kwa umma;

“Tunamtaka Pinda atakapojionea kwa macho athari za mgogoro huo umedumu kabla na baada ya mwaka 2006, achukue hatua za kinidhamu kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Umbulla na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mutagurwa, amshauri Rais Kikwete awafute kazi wote wawili mara moja”.ilisema sehemu ya taaraifa hiyo.

No comments:

Post a Comment