Na Bryceson Mathias, Mtibwa Mvomero.
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemnyoshea Kdole Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka, akidai uamuzi wake wa kufunga Kiwanda cha Mtibwa hadi kitakapolipa madeni ya wakulima na Wafanyakazi , ‘amekurupuka’.
Mbowe alitoa kauli hiyo leo (jana) kufuatia malalamiko ya wananchi walioshitushwa na uamuzi wa Serikali kupitia kwa Mkuu wa wilaya hiyo, kuamua kufunga kiwanda badala ya kumnyang’anya kutokana na Mwekezaji huyo kudaiwa na wakulima na Wafanyakazi zaidi ya Sh. Bilioni 1.2/-
Akihutubia umati wa wananchi wa Mji Mdogo wa Madizini na vitongoji vyake, Mbowe alimnyoshea Kidole Mkuu wa wilaya Mtaka akisema, “Madeni anayodaiwa Mwekezaji huyu, suluhu yake siyo kufunga Kiwanda, bali Serikali iltakiwa kutafuta fedha ya kuwalipa wakulima na Wafanyakazi hao.
“Katika hili DC amekurupuka, wakulima na Wafanyakazi wanataka Malipo yao, habari ya uamuzi wa kufunga kiwanda, ni kumnusuru mdaiwa asiwajibike, na wala haisaidii dai la msingi la wananchi, hivyo kilistahili ni Malipo na kuiangalia adha hiyo kitaifa maana inahusisha watu wengi”.alisema Mbowe.
Mbowe aliwaita viongozi chadema wamwambie malalamiko ya wananchi ili wamtune Kambi upinzani bungeni ikamhoji Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambapo Diwani wa Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, alieleza Manyanyaso, Dhuluma na ucheleweshaji wa Malipo yanayofanywa na mwekezaji dhidi ya wananchi na kuahidi kuyafanyia kazi.
Mbali na Mbowe kusisistiza tena kuhusu kuboreshwa kwa daftari la kura na mchakato mzima wa Katiba, ameendelea kudai, lisipoboreshwa daftari hilo Chadema haitakuwa tayari kuingia katika kura ya maoni, ila itarudi kwa umma kuwataka kususia mchakato huo, unaokumbatiwa na CCM.
Halima Mdee awahamasisha akina mama kuikataa CCM.
Aidha Mbunge wa Kawe Halima Mdee, akiambatana na, Suzan Kiwanga, amewataka akina mama wilayani Mvomero kuikataa CCM na Propaganda zake kwa sababu kila adha wanayoipat ikiwa ni pamoja na kupora ardhi kunakofanywa na vigogo wastafu wa CCM na walioko madarakani, madhara yake ni kwao hivyo waungane kuikataa CCM na kuichagua Chadema.
No comments:
Post a Comment