Jana majira ya saa 3.30 asubuhi, watu wapatao watano ambao ni wanachama wa CHADEMA mamluki wa Timu ya Zitto na CCM, wakiwa eneo moja la ofisi ya umma wakisubiri huduma ya muhimu sana, walipokea simu ya taarifa kuwa Mwenyekiti wao wa chama wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick alikuwa amekutwa mahali fulani Dar es Salaam baada ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa na watu wasiojulikana.
Wale watu mara tu baada ya kupokea habari hizo, wakamtafuta mtu waliyekuwa wakimwita kwenye simu jina la Mchange (wala si mwingine ni Mhange huyo huyo anayefahamika katika masuala hayaya circles za usaliti dhidi ya CHADEMA).
Wakamwambia habari hiyo (inavyoonekana yeye alikuwa tayari anaijua na alikuwa mahali fulani kwa mwanasheria). Akawauliza wanaweza kumtaja mtu (a watu) yeyote wanayetaka ahusishwe kwenye tukio hilo kisha afunguliwe kesi. Mtu ambaye akihusishwa itakuwa rahisi kwa viongozi wakuu wa chama na hatimaye chama kizima kuhusishwa kwenye tukio hilo.
Wale watu wakamwambia ili kumalizana na ‘biashara’ ya CHADEMA kabisa kwa kuwahusisha viongozi na hatimaye chama kizima katika tukio hilo ambalo linaweza kukuzwa na kuoneshwa kuwa ni UGAIDI, wako tayari kumtajia majina ya watu wawili ambao wamekuwa wakikihami na kukitetea sana CHADEMA Temeke, hivyo ni kikwazo kwa mikakati yao ya kukihujumu CHADEMA katika eneo hilo.
Kama inavyojulikana kwa upande wa Dar es Salaam, mikakati ya kuihujumu CHADEMA imekuwa ikifanyika kwa kiasi kikubwa sana Temeke.
Wale watu wakamtajia huyo mtu waliyekuwa wakimtaja kwa jina la Mchange, majina ya watu wawili, Mzee Salum Zinga na Bernard Mwakyembe. Wote hawa ni makamanda kweli kweli hapo Temeke, kiasi kwamba Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Wilaya ya Temeke amekuwa akimhofia sana Mwakyembe kwamba anaweza kuchukua nafasi yake wakati wa uchaguzi ujao wa ndani ya chama hicho.
Baada ya kumtajia majina hayo, wakamwambia wanapitia ofisi ya wilaya ya chama hicho mara moja, kisha wakutane kituo cha polisi ili wakafungue malalamiko dhidi ya watu hao wawili kuwa wamehusika na tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa mwenyekiti huyo. Mpango mzima ukawa umekamilika na ukatekelezwa.
Tunavyozungumza hapa sasa tayari Mzee Salum Zinga ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Temeke ameshakamatwa na polisi na sasa jeshi hilo linamtafuta Mwakyembe. Lakini kwa namna ambavyo mpango huo umepangwa na utakavyotekelezwa, lengo ni kuwafikia viongozi wa juu.
Mpango huo uliozungumzwa na watu hao watano pale Temeke kwa kuwasiliana na Mchange ndiyo msingi wa kauli za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova, kutamka kwa kuihusisha CHADEMA huku akijigamba kuwa watamkamata mtu yeyote bila kujali cheo chake. Akilenga viongozi wakubwa wa chama hicho.
Huyo Kova ambaye kwa sababu ameshajitambulisha kuwa ni bingwa wa kugeuza matukio haya ya ukatili kuwa ni ‘filamu’ ya kuficha ukweli na kuanza kusaka uongo, hatuna haja ya kumjadili zaidi ya hapo. Ila ajue tu kuwa mpango mzima unajulikana.
Ndiyo maana sehemu ya mpango huo ni kumlazimisha Yona arudi na kulazwa Moi ambako alikuwa ameagwa jana hiyo hiyo baada ya kubainika hana majeraha makubwa na angetakiwa kurudi baada ya wiki mbili. Hiyo ilikuwa ni baada ya CHADEMA kuwa wamesimamia matibabu yake, ikiwemo kumlipia gharama za hospitali na usafiri kumpeleka nyumbani.
Akiwa hapo hospitalini amezungumza na vyombo vya habari kwa namna tofauti tofauti, kwa mtazamo wa kila chombo na kadri ya maelekezo…
Mpango mzima unaandaliwa pia kupitia vyombo vya habari;
Angalia kutoka magazetini
Kama mlivyoona leo kwenye kurasa za mbele za magazeti yote yaliyotoka leo, habari hii imepewa uzito mkubwa, ingawa kwa namna tofauti tofauti, kulingana na uwezo, sera za vyombo vya habari na MALENGO ya chombo husika, hasa katika kufanya kazi za watawala dhidi ya CHADEMA.
Lengo lingine ni kubeba agenda za makundi ya kuwania urais ndani ya CCM, ambayo CHADEMA ndiyo tishio pekee la wao kufanikiwa kwenda ikulu, hivyo yanafanya kila jitihada kukiumiza chama hicho kwa propaganda nyepesi kama ya tukio hilo.
Kwa upande wako fanyia kazi PICHA zilizotumika leo katika magazeti yote. Zimepigwa wakati gani? Eneo gani? Saa ngapi huyo mpiga picha maalum alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kupiga hizo picha zinazooenakaana kupigwa kwa ustadi na kifaa kizuri? Kuna maswali mengi sana ukizingatia kuwa picha zilizotumika katika habari hiyo ni za aina moja! Nani kazipiga?
Hapa tunaweza kujadili habari kutoka katika magazeti kadhaa;
Endelea......
Mtanzania
Gazeti hili limeipatia habari hii kichwa kisemacho INATISHA. Ndani ya habari gazeti hilo kwa malengo linalojua yenyewe, labda likiongozwa na kile kinachoweza kuitwa aina ya weledi wa aina yake wa taaluma ya habari, sera za chombo hicho na malengo ya wamiliki, limewahusisha viongozi wa CHADEMA katika tukio hilo kwa hali ambayo inaacha maswali mengi sana.
Mathalani kwenye moja ya nukuu zake, wamemnukuu Yona akisema
“Bernard na Mwakyembe walinisalimia na kuondoka, baada ya hapo, wakaja watu wengine wane ambao siwajui, wakajitambulisha kwangu kuwa ni polisi wanatoka kituo cha kati, hivyo basi wananihitaji kwa ajili ya mahojiano.”
Waandishi wa gazeti hili wangekuwa na nia ya kufanya uandishi unaowajibika kwa jamii, wangefanya kazi yao kidogo tu wangebaini kuwa Yona katika hilo alikuwa amewadanganya au amewaambia kitu ambacho kinahitaji kufanyiwa kazi zaidi.
Kwa sababu kama umefuatilia mtiririko wa taarifa hii, kuna mtu anaitwa Bernard Mwakyembe (mtu mmoja), lakini hapa Yona ametaja kwamba hao ni watu wawili tofauti. Gazeti lilipaswa kufanya kazi yake badala ya kutumika kuwa karatasi ya kufanyia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA.
Katika aya mbili zinazofuata ndiyo zinaliacha gazeti hilo uchi kabisa kwamba limeamua kutumika kwenye mkakati unaoandaliwa na CCM kupitia vyombo vya dola. Limeandika hivi;
“Tulibishana sana tena ni muda mrefu, mwisho nikawaambia wanionyeshe kibali cha kunikamata lakini walinijibu kuwa wao ni polisi, napaswa kutii amri kama kuna mahojiano zaidi yatafanyika kituoni, nikapanda gari lao na kuondoka,” alisema Patrick.
Soma na aya inayofuata ambayo gazeti hilo limeandika kama vile lilikuwepo wakati tukio linatokea. Kwa sababu lilipaswa kuandika maneno ya Yona ni madai…allegations.
“Alipohoji sababu ya watu hao kujitambulisha ni polisi wakati anawajua kuwa si wanausalama, walianza kumshurutisha kuingia ndani ya gari alipogoma walimsukuma kwa nguvu ndani ya gari hilo na kumwambia kuwa wanampeleka kituo cha kati.”
Aya hizo mbili zilitosha kabisa kuwashtua waandishi au wahariri makini kuwa chanzo cha habari wanachozungumza nacho si cha kuaminika au kinazua maswali mengi mno.
Mtu aliyesema dakika kadhaa tu zilizopita kuwa walikuja watu wengine wanne hawajui, wanajitambulisha kuwa ni polisi, akawahoji vitambulisho, wakashindwa kutoa, akabishana nao sana maeneo ya baa (hakuna mtu aliyesikia?), cha ajabu akakubali kuondoka nao wakati yeye hawajui ni akina nani, ghafla tena anasema kuwa anawajua kuwa si wanausalama. Kuna maswali mengi sana?!
Kwa ujumla habari nzima ya Mtanzania kuhusu tukio hili, ilistahili kuandikwa na yale magazeti ‘crap’ ya ajabu ajabu yaliyoko mtaani, chini ya waandishi na wahariri ambao hawajui wala hawathamini chembe hata moja ya maadili achilia mbali weledi wa kitaaluma.
Wameandika habari ile badala ya kutumia madai ya nafsi ya tatu umoja, wao wameandika kama vile walikuwepo hatua kwa hatua na mlalamikaji Yona, lengo zima ikiwa ni kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na chama hicho katika sakata zima. Je Mtanzania maslahi yao katika hili ni yapi? Bila shaka ni makubwa sana.
Angalia aya hizi zilivyoandikwa kwa makusudi, kimkakati;
Patrick ambaye ni rafiki wa karibu na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto alisema kuwa mgogoro wake na viongozi wakuu wa chama hicho ulianza tangu alipoitisha mkutano na waandishi wa habari wa kuitaka Kamati Kuu ya chama hicho kuitisha mkutano wa kujadili suala la kina Zitto, Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo.
“Niliitisha mkutano ule ili kuwaambia viongozi wa CHADEMA kujadili suala la kina Zitto, Kitila na Mwigamba ndani ya chama na si kuwavua uanachama kama ilivyojitokeza jambo ambalo lilipingwa na viongozi wa chama hicho,” alisema Patrick.
Alisema, kutokana na hali hiyo viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa alimwita na kumuambia aache urafiki na Zitto la sivyo watamfukuza uanachama. (Walimwita lini, wapi kwa namna gani, hivi kweli viongozi wa juu namna hiyo wanaweza kumwita kiongozi wa wilaya hivi hivi tu, hicho chama si CHADEMA labda CHAUMA na viongozi hao hawawezi kuwa Mbowe wala Slaa, lakini kibaya kabisa, gazeti wala halikuwatafuta kutaka kujua upande wao na kupata hata ukweli. Uandishi wa hatari sana huu)
“Waliniita na kuniambia niachane na Zitto, nilipinga ndipo waliponiambia nijiondoe ndani ya chama hicho, niliendelea kupinga,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi hao walimwambia aitishe mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya na kuwaambia wajumbe wa kamati kuwa yeye si rafiki wa Zitto na kwamba hawezi kumuunga mkono kwenye harakati zake, lakini aliendelea kukataa suala hilo. (Hivi gazeti makini linaweza kunukuu uongo kama huu na kusema limeandika habari kwa ajili ya watu kusoma. Kuna tofauti gani na magazeti ya Yule jamaa mtunga hadithi).
“Tangu nilipoitisha mkutano wa waandishi wa habari wa kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama akina Zitto, Mwigamba na Kitila, nimekuwa kwenye mvutano mkubwa na viongozi wangu wa juu, nimepokea vitisho vingi ambavyo nilivirekodi kwenye simu yangu ya mkononi waliyoichukua,” alisema Patrick.
(Kwa trend ambayo chanzo hicho kimeonesha tanguy huko juu, huna haja ya kwenda hata darasa moja kujua kuwa huu ni uongo mkubwa unaosemwa na mtu anayejifunza kuzalisha fitna na majungu, lakini pia mwanafunzi wa kutengeneza mgogoro, lakini kikubwa kupika kesi. Mathalani mhariri makini hawezi kupitisha uchafu kama huu uwe habari, angeuliza tu, huyo Yona alifanya huo mkutano lini?, Ulihusu nini? Je ni kweli ulihusu kupinga kuwavua uanachama watu hao? Kwa nini kutumika kuandika uongo?).
Aliongeza, suala hilo liliendelea hadi Dk. Slaa na Mbowe walipomwita na kumlazimisha aitishe tena kikao kingine cha kamati tendaji ili atangaze kujiuzulu mwenyewe nafasi yake kabla ya kumfukuza uanachama, jambo ambalo alilipinga tena. (Umakini wa waandishi na wahariri wa gazeti hilo haukuwatuma kuona umuhimu wa kuwatafuta viongozi hao walau wahalalishe huo uchafu walioamua kuuita ni habari ya kuwapelekea Watanzania. Hii ni hatari sana.)
“Dk. Slaa aliniandikia barua ya kunitaka niitishe mkutano nilipoona kelele zinazidi nikaamua kuitisha lakini wajumbe wa kikao nilichoitisha kwa pamoja wakaniunga mkono na kusema wana imani na mimi, hivyo basi hawataki niondoke.
“Baada ya hapo, Dk. Slaa akaniandikia barua na kuniambia kuwa kikao nilichoitisha ni batili na kwamba wanatakiwa kuitisha kuitisha kikao kingine Januari 10 mwaka huu.”
Kwa ujumla habari nzima ya Mtanzania ni crap. Na kuonesha dhahiri malengo na nia ovu waliyonayo dhidi ya CHADEMA kupitia tukio hilo la kusikitisha la kutekwa na kuteswa kwa Yona, gazeti hili ambalo limeandika mengi sana ya KUUMIZA, yanayokiuka maadili na weledi wa uandishi, likimnukuu mwenyekiti huyo akisema uongo dhidi ya Mbowe na Dk. Slaa, halikuwatafuta viongozi hao, lakini likamtafuta Zitto Kabwe.
Wanaandika hivi;
“Nikiangalia tukio langu na mgogoro uliopo ndani ya chama najua nimeumizwa kwa ajili ya kumtetea Zitto, kwa sababu nimekuwa nikipokea vitisho kutoka kwa viongozi wa juu wa chama na M4C,” alisema.
Kukamilisha mpango huo wa spinning ya kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na hatimaye chama kizima katika sakata hilo, Zitto akatafutwa na akasema hivi;
Akizungumzia tukio hilo, Zitto amesema vurugu kamwe siyo suluhu ya siasa nchini na kwamba ni kitendo kinacholenga kuwaingiza watu katika woga na kuwatisha.
“Haya ni matendo ya kikatili na ya kumuogopesha kutokana na kupinga baadhi ya mapendekezo ya upande wa baadhi ya viongozi Kamati Kuu ya chama.
“Natoa changamoto kwa viongozi zote wa Chadema kwamba sasa wakanushe kuwa vurugu siyo silaha yao katika siasa,” alihitimisha Zitto.
Huyu mtu tayari alishajua na kuhitimisha kuwa viongozi na chama chake kinahusika na tukio hilo? Kwa nini anawahi kuhitimisha kuwasukumia tukio zito kama hilo ambalo linaweza kuharibu kabisa chama chake ambacho eti anataka kuwa mbunge na kiongozi wake. Au ni mwendelezo wa mkakati ule ule, wakakutanishwa kwenye kipindi cha Star tv asubuhi yeye na Mwigulu, Mwigulu Nchemba akajifanya anatoa habari ya ugaidi wa CHADEMA?
Habari za kiuchambuzi juu ya mkakati huu wa kutaka kurudisha taswira ya ugaidi na kuihusisha CHADEMA na matukio ya vurugu yanayohusisha umwagaji wa damu ikipangwa kwa ustadi na wale wale, kwa mtindo ule ule, kwa malengo yale yale, zitaongezwa baadae katika andiko hili;
Kazi ipo watanzania tutapumbazwa sana na hili kundi la wachache kakini kumbuka ''Every dog has it's day'' Mungu ibariki Tanzania mungu wabariki wanyonge.
ReplyDeleteNdg mwandishi, makala yako ni muhimu sana kwa mustakabali wa CHADEMA, ni muhimu kwa vyombo vya usalama hususani TISS na Polisi. Napendekeza uichapishe katika magazeti ili isomwe na wengi na unafiki wa gazeti la Mtanzania pamoja na Zitto Kabwe uwe wazi zaidi
ReplyDelete