Sunday, December 22, 2013

Wajumbe Kamati Kuu CHADEMA wamuonya Zitto.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA wamemuonya aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe kwa ukiukwaji wa waziwazi wa taratibu za chama hicho.
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wajumbe hao wameshangazwa na kitendo cha Zitto Kabwe kujiandalia ziara zenye mwelekeo hasi kwa chama hicho.
Ikumbukwe kwamba Zitto amefukuzwa nafasi zote za Uongozi ndani ya Chadema na yeye ni mbunge tu wa Kigoma Kaskazini huku akisubiri huruma ya Kamati Kuu kuhusu uanachama wake.
Kilichoshangaza zaidi ni kitendo cha Zitto Kabwe kufanya ziara Jimbo la Kasulu bila kutaarifu Chama huku mashabiki wake wakiutumia mkutano huo kukashifu chama na viongozi wake.
Kitendo kinachofanyika hakikubaliki na ni ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za chama.
Katika hali ya kuonyesha kinachofanywa ni mkakati wa kuangamiza Chadema Gazeti la Jamboleo Toleo la Jumapili linalomilikiwa na Kada wa CCM katika habari kuu limeandika "Zitto aimaliza CHADEMA" likiripoti yanayotokea Kigoma.

No comments:

Post a Comment