Friday, October 4, 2013

Dr. Slaa Atembelea Moja Ya Bandari Kubwa Marekani !

Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania” ambayo leo imemfikisha moja ya bandari kubwa nchini marekani. Bandari ya Mobile Alabama ambako alipokelewa na mkurugenzi wa Shirika la Alabama Ports Authority


Shirika la Alabama Ports Authority inapitisha makontena 100 kwa lisaa limoja na mizigo inayozidi tani million 30 kwa mwaka na kuipa shirika hilo linalojitegemea kiasi cha dola za kimarekani million 152 kwa mwaka ambazo ni faida. Shirika hilo lina wafanya kazi 600 tu, lakini imeweza kutoa ajira ambazo siyo za moja kwa moja 280,000.



Bandari ya Alabama inajitegemea kiuendeshaji; haliingiliwi na uongozi wa jimbo. Utekelezaji wa bandari hii ni wa kipekee kwa sababu mizigo uondoka bandarini punde tu zinapowasili au chini ya siku tatu. Alichojifunza Dr. Slaa katika ziara hii ni kwamba, mashirika ya umma yanaweza kufanya kazi kwa ufaninisi mkubwa pasipo uingiliaji wa kisiasa.



Dr. Slaa pia amejifunza kwamba, kama jimbo dogo kama Alabama inaweza kupitisha tani million 30 kwa mwaka, basi Tanzania inaweza kupitisha tani million 100 kwa mwaka kutokana na jiographia yake. Dr. Slaa anaamini kwamba Bandari ya Tanzania inaweza kuajiri vijana 350,000 chini ya utawala wa Chadema.



Dr. Slaa anaamini kwamba, mashirika ya umma kama bandari hayana ufanisi kwa sababu waendeshaji wake wanateuliwa kiurafiki na kindugu bila ya kuzingatia uwezo wa mtu. China ya utawala wa Chadema haya yote yatafikia kikomo kwa manufaa ya watanzania wanaoumia na umasikini


Alabama Business Council.

Dr. Slaa amekutana na viongozi wa juu wawili wa “Alabama Business Council” Katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili yake na taasisi hiyo. Mwenyekiti wa Alabama Business council ameahidi kuhamasisha makampuni makubwa kwenye jimbo la Alabama kumsaidia Dr. Slaa na Chadema kunyunyua uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza kwenye sekta mbali mbali za uchumi wa Tanzania kama Kilimo, elimu, viwanda, miundombinu nishati nk.












1 comment:

  1. Dr.Slaa umelamba dume,wamerekani wakikukubali hata mbinguni umekubaliwa.

    ReplyDelete