Akimkaribisha Dr. Slaa katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “
Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo. Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.
Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu. Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football.
Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania. Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo.
Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa. Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha.
Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Dr. Slaa
Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani akisalimiana na Dr Slaa
wakiwa katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo, Dr. Slaa alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani
Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye
Msafara wa Dr. Slaa ukiwasili uwanjani
Mshindi wa Nobel Peace Price na Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno
Viongozi Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Dr. Slaa ndiye mgeni Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri
Uwanja ukiwa umefurika wapenzi wa mpira takribani laki moja
No comments:
Post a Comment