Wednesday, October 16, 2013

CHADEMA Kanda Ya Kaskazini: Taarifa kwa umma/wadau


TAARIFA KWA UMMA/WADAUTAREHE 15 OKTOBA 2013


MKUTANO WA BARAZA LA UONGOZI LA KANDA YA KASKAZINI NA WADAU WA CHADEMA WAPENDA MABADILIKO NA UHURU WA KWELI.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kinapenda kuwatangazia na kuujulisha umma na wadau wote kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kuwa tarehe 25 hadi 27 Oktoba 2013 katika JIJI la Arusha yalipo makao makuu ya chama kwa kanda, kuwa kutafanyika mkutano wa Baraza la Uongozi la Kanda tarehe 25 Oktoba, ambalo
litajumuisha viongozi wa mikoa na mabaraza ya chama ngazi ya mikoa kutoka kanda ya kaskazini, Wabunge wote kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri zilizopo chini ya CHADEMA kutoka kanda ya Kaskazini na wajumbe wa kamati kuu wanaoishi ndani ya kanda ya kaskazini.

Sambamba na mkutano huu wa baraza la uongozi, tarehe 26 na 27 Oktoba, utafanyika mkutano wa wadau wote wa chama na wapenda mabadiliko ya kweli kutoka kanda ya kaskazini. Wadau hawa ni pamoja na wanasheria wote, wachumi, wahasibu, wahandisi, wahadhiri wa vyuo na waalimu, wanahabari, wafanyabiashara, viongozi wa dini na makundi yote maalumu na ya kitaaluma, wote wanaalikwa kushiriki katika mkutano huu ambao una lengo la kutoa fursa kwao kama watanzania wakiwa kama wadau wa kweli waweze kuitumikia nchi yao kupitia CHADEMA.

Katika mkutano huu wadau watapata fursa ya kushirikishwa katika nafasi za kimaamuzi na kiutendaji za kanda kwa lengo la kuijenga na kuiimarisha CHADEMA ambayo imekuwa na imeendelea kuwa tumaini kwa Watanzania kwa wakati huu wa uhitaji mkubwa wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.

Mkutano huu utafunguliwa na pia kuhudhuriwa Mwenyekiti wa CHAMA Taifa Mhe Freeman Mbowe (MB) ambaye pia ni mbunge kutoka Kanda ya Kaskazini.

MAWASILIANO yote yafanyike kupitia kwa MRATIBU - KANDA
Ofisi ya KANDA – ARUSHA – Ngarenaro: NHC Nyumba Na. 8
S.L.P. 12525, Arusha, Tanzania. Simu: +255 784 343 275,
Email: chademakaskazini@gmail.com Tovuti: www.chadema.or.tz
Wadau wote mnakaribishwa sana kuhudhuria mkutano huu.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ushiriki kwenye mkutano huu tafadhali tumia mawasiliano kwa
njia zifuatazo:
Simu: +255 758 976 260
+255 656 557 586
+255 755 282 878
Barua pepe: chademakaskazini@gmail.com
golugwa@gmail.com
Imetolewa leo tarehe 15 Oktoba 2013
Amani S. Golugwa
KATIBU – KANDA YA KASKAZINI

No comments:

Post a Comment