Operesheni maalumu ijulikanayo kama “Giant Mgimwa” itakayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Nyanda za Juu Kusini, kwa lengo la kumshitaki kwa wananchi Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, itaanza kesho.
Operesheni hiyo itakayohitimishwa Oktoba Mosi, mwaka huu, itafanyika katika kata zote 13 za Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, linalowakilishwa bungeni na Waziri Mgimwa.
Kaimu Ofisa Habari wa Chadema jimboni humo, Aidan Salehe, alisema watafanya hivyo kupinga kitendo cha Waziri Mgimwa kushiriki katika kuanzisha tozo ya kodi kwa laini za simu, ambayo itawaumiza wananchi.
Alisema katika mikutano hiyo wanatarajia kupokea wanachama wapya 4,500 kutoka CCM, ambao alisema watapokelewa na Mratibu Kanda, Frank Mwaisumbe, ambaye ataongoza msafara utakaoshirikisha wabunge; Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na David Silinde (Mbozi Magharibi).
No comments:
Post a Comment