Tuesday, July 30, 2013

CHADEMA yavuna wanachana 300 Tanga

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Tanga kimepata wanachama wapya zaidi ya 300.
Wanachama hao wamepatikana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za Handeni, Muheza na Korogwe uliohutubiwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje.
Wanachama 220 wamejiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kwengoma, Kata ya Kwamatuku, Wilaya ya Handeni na wanachama 71 ni kutoka Kibanda, wilayani Muheza.
Wanachama wengine 21 akiwamo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Turiani, Bakari Kimea walijivua uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwashemshi, Wilaya ya Korogwe.
Wakizungumza katika mikutano hiyo baada ya kujiunga na CHADEMA, walisema wameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kimeshindwa kuondoa kero zinazowakabili kwa miaka mingi.
Miongoni mwa kero hizo kwa mujibu wa wananchi hao ni unyanyaswaji unaofanywa na viongozi wa serikali za vijiji, kunyang’anywa ardhi, kero ya maji na kuvunjiwa mikataba na muwekezaji.

No comments:

Post a Comment