Saturday, July 27, 2013

CCM Kikombo yakanusha kutafuna fedha za Mnara wa Airtel.

Na Bryceson Mathias, Kikombo, Dodoma vijijini.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Kikombo, Kata ya Kikombo, Manispaa ya Dodoma, kimekanusha vikali tuhuma zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba, fedha za malipo ya Mnara Sh. Mil 2/= zilizolipwa na Airtel zimetafunwa.
Akijigamba na kumtishia mwandishi jana Julai 27, kwamba yeye ana fedha ya kutosha ya biashara, Mwenyekiti wa Kijiji, Petro Kusena, aliruka futi 100 akidai kauli zilizotolewa na Chadema katika mkutano uliofanyika uwanja michezo shule ya Kikombo, ni za uchochezi.
Kusena alikanusa tuhuma hizo baada ya aliyekuwa Mgombea wa Udiwani, Yona Kusaja, na baadhi ya wananchi katika Mkutano huo, kuwa waliwataka wajiuzulu nyadhifa zao kwa kushindwa kujenga Madarasa matatu yaliyoezuliwa 2010, wakidai Mil. 2/- zilizokusudia ujenzi huo, zimelambwa.
“Mwandishi, Ofisi inao muhutasari na taarifa ya mapato na matumizi ya fedha hizo kimaandishi, fedha zilitumika kwa Ujenzi wa Madarasa matatu ya Shule ya Ngungu, kwamba tumezitafuna, hiyo ni lugha ya uchochezi kwa watu walioshindwa uongozi”.alisema Kusena.
Mapema katika moja ya vikao wananchi waliwakataa Mwenyekiti Kusena, na Mtendaji anayekaimu, Wello Dede, wakitaka wajiuzulu na kuwajibika kwa tuhumu za kutosoma mapato na matumizi, na kwamba wameshindwa kusimamia rasilimali zao, lakini bado wameng’ang’ania.
Aidha Mtendaji Dede alisema, fedha hizo Mil 2/- zimenunua Saruji mifuko 70 ya kujenga Msingi na Karo la Vyumba Vitatu vya Shule ya Ngungu, na aliahidi Uongozi utasoma mapato na matumizi hivi karibuni.
“Uongozi tunanafuatilia mtandao wa tiGo ambao wamejiunganishia Mnara wao kwa Airtel tulioingia Mkataba nao, bila kutupa taarifa, ikiwa ni kinyume na Mkataba na mteja wetu Airtel Uk.4 (5) kwa lengo la kutudhulumu na kutuhujumu”.alisema Dede.

No comments:

Post a Comment