Taatizo la ajira nchini kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya mfumo
haramu wa elimu ambao kwa makusudi umekumbatiwa na serikali ya CCM kwa manufaa
yao ya kujidhatiti madarakani.
Mfumo wa elimu uliopo na kiwango duni cha elimu kinachotolewa
kinazalisha vijana zaidi ya 800, 000
kila mwaka wasio na uwezo wa kuajiriwa popote na hata kijiajiri kwa chohote
Serikali ya CCM imekosa akili na maarifa ya kutambua kuwa
elimu bora inayokidhi mahitaji ya taifa ndio njia mojawapo na muafaka kutatua
tatizo la ajira nchini kwani fursa za ajira zimejaa duniani kote na
wanaozifaidi ni wale wenye maarifa na ujuzi ambao msingi wake mkuu unatokana na
elimu bora wanayoipata.
Kuonyesha kwamba serikali ya CCM imefilisikia fikra na maono
ya kulinasua taifa kutoka kwenye janga hili, sekta ya elimu sio kipaumbele
kwenye bajeti yake ya mwaka 2013/2014 na hata bajeti zilizopita. Kama taifa ni
lazima kuwekeza kwenye elimu kwa ufanisi na sio kwa ubabaishaji na usanii kama
huu unaofanywa na serikali ya CCM.
Sambamba na kushindwa kufanywa mapinduzi ya elimu nchini
Serikali ya CCM imeendelea kuwaweka vijana wa taifa hili rehani kwa kuendelea
kuuwa viwanda ambavyo kimsingi ni injini nyingine ya kutatua tatizo la ajira
nchini. Viwanda ndio sekta inayoweza kuajiri watu wa aina yoyote, wenye ujuzi
na wasio na ujuzi, wenye elimu na wasio na elimu, lakini Serikali ya CCM
imefubaa kimawazo kulitambua hili.
Kuimarisha sekta ya viwanda maana yake ni kuinua sekta ya
kilimo ambayo ni eneo muhimu la kutatua tatizo
la ajira nchini. Kwa kujenga uchumi wa viwanda maana yake utahitaji mali
ghafi ambazo zinazalishwa hapa nchini.
Kujenga viwanda vya kubangua korosho maana yake
unawahamasisha wananchi wa kusini walime kwa wingi korosho maana
unawahakikishia soko la korosho zao. Kujenga viwanda vya kusindika matunda
maana yake unawahamasisha wananchi walime kwa wingi matunda kwa kuwa
unawahakikishishia soko la matinda yao. Kujenga viwanda vya nguo maana yake
unawahamasisha wanachi walime kwa wingi pamba kwa kuwa unawahakikishia soko la
pamba yao n.k
Taifa linahitaji uongozi mpya wenye maono mapya ili kujenga taifa
bora na hili haliwezekani chini ya chama na serikali inayojifia ya CCM.
Ni fedhea kuwa na serikali ya watu waongo wenye kutoa ahadi
za adaha kwa wananchi hususani vijana.
Mwaka 2010, Rais Kikwete alihaidi kujenga machinga Complex
zaidi kwenye manispaa za Kinondoni na Temeke, akidai zitasaidia kutatua tatizo
la ajira lakini mpaka leo hii hakuna cha hizo zinazoitwa Machinga Complex
ukiacha ile pale Ilala ambayo inafuga panya na popo mle ndani. Maana yake Rais
ni muongo!
Serikali imebaki kukimbazana kwa mabomu na vijana mitaani
ambao wameona njia ya kujiaajiri wenyewe ni kufanya umachinga. Chini ya
serikali mufilisi ya CCM, vijna wanoenakana ni nuksi mijini, wachufuzi wa miji
nk. Kama serikali haitaki haya iwekeze kwenye elimu, ijenge uchumi wa viwanda,
ifanye mapinduzi ya kilimo jambo ambalo ni dhahiri hata ashuke malaika serikali
hii haitaweza kufanya hivyo.
Hivyo ni muhimu vijana kufanya mabadiliko ya msingi na
mabadiliko haya ni kuondoa uongozi wa CCM uliopo ambao hauna wazo lolote jipya
na kupata serikali ya mpya ya chama kipya chenye mawazo mapya na njia mbadala
za kushughulikia matatizo ya vijana na jamii kwa ujumla nchini. Serikali hii na
chama hiki ni CHADEMA.
Kufanya mabadiliko haya ni muhimu vijana popote mjitikeze
kugombea na kushika nyadhifa za serikali za vitongoji, vijiji na mitaa mwakani
kupitia CHADEMA na udiwani na ubunge mwaka 2015
Deogratias Munishi
Katibu Mkuu -BAVICHA
No comments:
Post a Comment