Tume ya Uchaguzi ya Taifa imetangaza kuahirisha uchaguzi mdogo wa Madiwani uliokuwa ufanyike tarehe 30.06.2013 katika Kata nne -Elerai, Themi, Kaloleni, Kimandolu- za halmashauri ya Manispaa ya Arusha.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema badala yake uchaguzi huo utafanyika tarehe 14 Julai 2013.
Amesema sababu kubwa ya kuahirisha tena uchaguzi huo ni kuwapa wananchi muda wa wiki mbili zaidi za kutulia kutokana na taharuki iliyotokea katika mkoa huo siku chache zilizopita, hali ambayo inaweza kuathiri upigaji kura na matokeo.
Uchaguzi huo awali ulipangwa ufanyike Jumapili ya terehe 16 Juni 2013, lakini uliahirishwa baada ya kutokea shambulio na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CHADEMA, siku ya Jumamosi ya tarehe 15 Juni 2013, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine wawili siku chache baadaye.
No comments:
Post a Comment