BAADHI ya Wazazi, Walimu na Wananchi walio wengi wa Vikindu, Kisima na Tambaani Wilaya ya Mkulanga, wamekiomba Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) na viongozi wake, kuwanusuru na dhuluma ya Zao la Korosho na Ufisadi wa Fedha za Ujenzi wa Sekondari.
Ombi hilo walililotoa June 1, mwaka huu walipozungumza na Mwandishi kwa nyakati tofauti, ambapo walitoa Kilio chao wakidai, Kutokana na kukopwa na kudhulumiwa bei ya zao lao la Korosho, hawana uhakika na maisha yao maana hakuna wa kuwatetea dhidi ya Uozo huo.
Mbali ya Kilio hicho, walisema wanakiomba Chadema na Viongozi wake, kuwatazama kwa jicho la tatu la huruma, ili wafike wilayani humo eneo la Vikindu, Kisima na Tambaani, ambako Fedha takribani Milioni 66/- za Ujenzi wa Nyumba za Walimu zimefujwa.
“Kwa hali ya Dhuluma ya Korosho zetu na Ubadhirifu wa Milioni 66/- uliofanywa na waliokuwa walimu wakuu waliopewa Uhamisho baada ya Uchafu huo, palipofikia sasa tunahitaji msaada wa Nguvu Mbadala ya CHADEMA”.alisema Mwalimu aliyeomba asitajwe.
Pia Walimu hao wamelaani kitendo cha Walimu wenzao wawili waliotuhumiwa na Ubadhirifu wa fedha za Ujenzi wa Nyumba hizo, kushushwa Vyeo vya Ualimu Mkuu na kuhamishiwa Shule zingine, huku wengine wenye makosa hayo hayo wakiachwa na kuhamishwa vituo tu!.
Mwananchi mmoja anayetaka Mabadiliko ili wakulima wa Korosho wasifanywe watumwa wa kuwazalisha Korosho na wengine wafaidi na kuomba pia asitajwe alidai, kunahitajika Mapinduzi makubwa ya mabadiliko ili watu wafikie mahali pa kupata Haki inayominywa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkulanga, Saada Mwaluka, alisema “Mimi ni Mgeni wilayani, hivyo sifahamu chochote kuhusu madai hayo, Ila nitafuatilia”.
Afisa Elimu Vifaa na Vielelezo (W), Mussa Ally, alikanusaha kufujwa Mil. 66/- za ujenzi za Nyumba za Walimu pekee, ila alikiri fedha hizo ni za Ujenzi wa Nyumba za Walimu, Ada na Michango, na kusema wahusika wana tuhuma za kujibu Hoja za Wakaguzi wa Ndani.
Aidha Kuhusu kushushwa Vyeo kwa baadhi ya Walimu na Uhamisho uliotolewa kwa upendeleo alidai,
“Unatokana na Walimu hao kukaimu nafasi hizo, ambapo walionekana wameshindwa kuonesha Uwezo wao wa Kitaaluma, Ushirikiano na Halmashauri, ambapo kila mmoja wao anatakiwa kujibu hoja (Query) za Wakaguzi, pale ambapo vithibitisho vya hati za malipo ya Ujenzi huo vilikosekana”.alisema Ally.
No comments:
Post a Comment