CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema, kitawatimua wanachama Mamluki wenye uroho wa Madaraka wanaotaka kutumia jina la chama kujinufaisha binasi badala ya kuwatumia wananchi wanaokusudiwa.
Hayo yamesemwa jana, Mei 31, mwaka huu na Katibu wa Tawi la Chadema Kata ya Mlaguzi Henred Barnabas kufuatia kurudishiwa Kadi ya CHADEMA na aliyekuwa Mhamasishaji wao Reuben Sembuche, ambaye kabla ya Uchaguzi mpya alikuwa Katibu wa Kata hiyo.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Barnard alisema, awali hata yeye alikuwa akishawishiwa na Sembuche ili aandike barua ya kujitoa Ukatibu na kurudisha Kadi ya Chadema, lakini hali akitaka kuwabaini wanaotumia vibaya jina la Chadema alikataa.
“Mwandishi, Ngoja nichaji simu yangu nikueleze Mkanda mzima wa Njama zinazopangwa na kutumiwa na watu waliokosa madaraka kwa lengo la kutaka kulitumia vibaya jina la Chadema ili kujipatia fedha, badala ya kuwatumikia wananchi”.alisema Bernard.
Aliongeza kusema, kuna Mamluki ambao ndani ya Chama ambao hawana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi, badala yake wamekuwa na Uroho wa kugombania Madaraka na Vyeo ili wavitumie kujipatia fedha kwa maslahi binafsi badala ya kuwakomboa wananchi na adha.
Mamluki hao wamebaini maamuzi magumu ya Chama yanayotarajiwa kuchukuliwa hivi karibuni, kutokana na watu wa namna hiyo ambao wamevaa ngozi ya uharibifu wa Chadema huku wakijidai ni wakereketwa wake kumbe ni waharibifu waliojificha nyuma ya mgongo.
Alipotafutwa Sembucha kwenye simu 0714260759 ili kutoa ufafanuzi kwa nini amerejesha Kadi ya CHADEMA, na tuhuma za kulitumia vibaya Jina la Chama kujipatia fedha badala ya kuwahudumia wananchi, simu yake iliita bila majibu, alipotafutwa Diwani wa Viti Maalum (CHADEMA) Kata ya Mtibwa, Juliana Petro, alikiri kusikia Sembucha amerudisha Kadi.
Na Bryceson Mathias, Mvomero.
No comments:
Post a Comment