Saturday, May 11, 2013

Mwimbaji wa Nyimbo za Siasa wa CCM atimkia CHADEMA


MWIMBAJI wa Nyimbo za Siasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mvomero, Haji Athumani Mbenzi, ameamua kuachana na Ukapera wa kuvaa Gamba na kuamua kutimkia Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) ili avae Gwanda.
Mbenzi ambaye amekipiga Pigo CCM alijisalimsha kwa CHADEMA katika Mikutano ya Mabadiliko ya M4C inayoendelea wilayani humo, ambapo hivi karibuni alifanya maamuzi magumu ya kukihama CCM na kujiunga na Chadema akidai anataka aimbe nyimbo za Ukombzi bila kuhaririwa na Magamba.
Akizungumzia uamuzi wake huo Mbenzi alisema, anasikitika kuchelewa kuungana na wapiganaji wenzake katika kuwaletea wananchi ukombozi wa haraka kutoka kwa watawala, lakini akadai, pamoja na kuchelewa atahakikisha anakimbia na M4C hadi awakute waliomuacha kwa kutumia Usanii wake.
“Najiona nimeachana na Ukapera wa kuvaa Gamba lililokuwa linanitesa ninapoimba nyimbo kwa tiketi CCM, hivyo naamini nitakuwa na mashambulizi mazuri nikiimba nikiwa nimebadilika kwa kuvaa Gwanda ambalo ni vazi la vita ya ukombozi wa Rasilimali za watu na Taifa”.
Aliyekuwa Mgombea wa Udiwani Kata ya Sungaji (CHADEMA) Jairosi Yohana Msigwa amethibitisha Mwimbaji huyo kjiunga na Kambi ya M4C tayari kwa mapambano ya kuikomboa Sungaji na Wilaya ya Mvomero toka Mafisadi wachache, ambapo amesema watakuwa naye wakishambulia Mlaguzi.
Viongozi na Wanachama CCM katika Mitaa, Vitongoji, Kata na Wilaya, bado hawaamini kilichotokea, hivyo wamebaki midomo wazi wakishangaa na kujiuliza, hivi kweli Mbenzi kaenda CHADEMA?  Wanapopewa Jibu ndiyo, wanabaki wakinungunika.
Aidha baada ya Chama cha CHADEMA kukumbatana misukosuko mikubwa ya Mkurugenzi wa Wilaya Mvomero Sarah Linuma, kukwamisha Mikutano ya Chama kwa kushirikiana na OCD Emmanuel Gariamoshi, kutokana na viongozi hao kuzibwa mdomo na Kashfa za upotevu wafeha za Wilaya kwa Mkurugenzi, na Malalamiko ya Wafugaji na Wakulima kwa OCD, wamefungwa kidhibiti mwendo, na CHADEMA inaonekana inaondoka.

No comments:

Post a Comment