Saturday, May 18, 2013

Mbunge wa Chadema Viti Maalum MWANAMRISHO ABAMA Augua Ghafla


MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Mwanamrisho
Taratibu Abama leo asubuhi aliugua ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali.
Tukio hilo lilitokea wakati akienda  kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu
Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu na kusaidiwa na wenzake
kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge.
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali
ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa.
Kwa mujibu wa waliomshuhudia,  alianza kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu
walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu kabla ya kupelekwa
hospitalini.
Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Dodoma,  Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.


No comments:

Post a Comment