Mbowe aongoza viongozi wa CHADEMA kuzuru majeruhi na eneo la Olasiti, Arusha
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe jana jioni aliwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013.
Baadaye katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Mbowe aliwapa pole wote walioathirika kwa janga hilo kwa namna yoyote, na kuwataka Watanzania wote wawe watulivu wakati vyombo vya dola vinafanya kazi yake, lengo likiwa ni kuwapata wahusika ili ijulikane hasa lengo lao.
Baada ya kutoka hopsitalini, Mbowe na msafara wake walielekea Elerai kuhani msiba mmoja wa waliofariki.
Mbowe katika msafara wake aliambatana na wabunge wa chama hicho kwa majimbo ya Arusha Mjini na Arumeru Mashariki, pamoja na viongozi wa juu wa Chama wa Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment