Mabadiliko
katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa chama cha
CUF....na kuishia na maneno…Israel
Liberal ‘ sasa isomeke:
“Mheshimiwa
Spika, kwa
upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama
hicho ni mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal
International). Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford
Congress ya Liberal International Mwaka 1997.
Mwaka huo huo Liberal
International ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto
(Ilani ya Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48
uliofanyika tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford
nchini Uingereza.
Katika ilani hiyo ya
waliberali, umoja wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the
extension of the rules of equality to sexual minorities and the recognition
that homesexuality and lesbianism are legitimate expressions of personal
proclivities”. Kwa Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya
waliberali katika karne ya 21 (The Liberal Agenda in the 21st
Century) ya kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali.
Hii ni kwa mujibu wa tangazo
la Umoja huo kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na
Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha
Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu
ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja. Kupitia umoja hao CUF
inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre
cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal………”
Ezekiah
Dibogo Wenje
Msemaji
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
30
Mei 2013
The message seems unaltered. Its OK!
ReplyDelete