Saturday, May 11, 2013

CHADEMA YATWAA VIGOGO WATANO WA CCM

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Chato mkoani geita,kimeendelea kukitesa chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli baada ya kutwaa vigogo watano wa chama hicho.

Hatua hiyo ambayo imetafsiliwa ni kuzivunja ngome za mbunge wa jimbo hilo, juzi Chadema kilifanikiwa kuwapokea Mabalozi watatu kutoka CCM,Mwenyekiti wa CCM tawi la Ilyamchele na mwenyekiti wa kitongozi cha Mwabasabi CCM Mathias Salala, ambao walilejesha kadi zao na kukabidhiwa za Chadema.

Waliokabidhi kadi za CCM na kutimkia Chadema katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Ilyamchele wilayani hapa na nyazifa zao kwenye mabano ni Boniphace William(Balozi),Titus Bufula(Balozi),James Nhabihabi(Balozi), Filmon Kasamwa (mwenyekiti wa CCM tawi,pamoja na Salala.

Hatua hiyo ilikuja baada ya aliyekuwa mjumbe wa Baraza kuu la jumuiya ya wazazi wa CCM taifa ,na mwenyekiti wa CCM wilaya ya geita,kabla ya kutimkia Chadema, Daudi Sunzu Ntinonu,kukishitaki Chama cha Mapinduzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe kwa madai wamegoma kuifungua shule ya sekondari Ilyamchele kutokana na kata hiyo kuongozwa na diwani wa Chadema Josephat Mayunga.

Ntinonu alisema kuwa mchezo mchafu uliofanywa na viongozi wa CCM kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chato kukataa kuifungua shule iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu katika kata ya Ilyamchele na kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kati ya kilometa 10 hadi 15 kwenda kusoma kwenye shule ya sekondari katende na Ilemela,ni kuwatesa wananchi na wala siyo Chadema.

Kwa upande wake mratibu wa vuguvugu la Mabadiliko la Chadema M4C wilaya ya Chato, Josephat Manyenye, aliwataka wananchi wa kata hiyo kuungana kwa pamoja na kupaza sauti zao kutokana na hujuma wanazofanyiwa na viongozi wa Chama tawala huku akiwaonya vikali watendaji wa chama na serikali ambao wamekuwa wakiwazuia wananchi wa kata hiyo kujitolea katika ujezi wa sekondari ya kata hiyo.

Alisema ni kitendo cha ajabu kuona baadhi ya viongozi wa CCM wanazuia maendeleo ya wananchi ali hali wao ndiyo wasimamizi wa Ilani inayotekelezwa na serikali iliyopo madarakani na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka misingi ya Chama chao.


Mwishoni mwa wiki katika kikao cha madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Chato wakati akijibu swali lililoulizwa na diwani wa kata hiyo, Ofisa elimu wa sekondari Hellen Kahindi alisema licha ya sekondari hiyo kuwa na vyumba viwili vya madarasa, vyoo matundu manne,Jengo la utawala, Ofisi za walimu,mazingira mazuri ya eneo la shule,na nyumba ya mkuu wa shule iliyo katika hatua ya linta bado wanatakiwa kukamilisha vyoo vingine vinne,thamani za ofisi,nyumba 2 za walimu, madawati na viti vyote vya madarasa hayo.


No comments:

Post a Comment