Sunday, April 21, 2013

Mbowe, Slaa wampa live Makinda


Hakutakuwa na amani, utulivu bungeni upendeleo ukiendelea!
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeonya kuwa hakutakuwa na amani na utulivu ndani ya Bunge iwapo, kiti cha Spika kitaendelea kuendesha bunge hilo kwa upendeleo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa, walisema jana mjini Dodoma, kwenye mkutano wa uzinduzi wa  mafunzo ya makamanda wa Chadema kanda ya kati, na kuongeza kuwa kufukuzwa kwa wabunge sita wa chama chao wiki hii ni  matokeo ya kuendesha Bunge kwa upendeleo  bila kuzingatia kanuni.
Wiki hii wabunge sita wa Chadema, Tundu Lissu-Singida  Mashariki,  Joseph Mbilinyi Mbeya Mjini,  Peter Msigwa –Iringa Mjini, Highness Kiwia, Ilemela , Godbless Lema –Arusha Mjini na Ezekiel Wenje-Nyamagana, walipewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano mfululizo vya bunge.
Adhabu hiyo ilitolewa na  Naibu Spika Job Ndugai, kwa kile alichodai kuwa  ni utovu wa nidhamu.

 Bonyeza Read More Kuendelea




Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Slaa, alisema kitendo cha kuwatimua makamanda hao ni kuonyesha upendeleo mkubwa kwa CCM na kupindisha kanuni.
“Spika anaendesha Bunge kwa kuelekezwa na CCM, haliendeshi kwa moyo, wala mapenzi yake, wala hatumii hekima au busara zake,” alisema.
Slaa alisema licha ya Lissu  kuwa nje ya Bunge yuko kazini na kazi yake ndani ya maoni ya upinzani kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais   Muungano  imesikika bungeni.
Mbowe alisema wabunge hao wamekataa kuwa kondoo na kutii uongozi usiotenda haki.
Alisema kama Bunge linavyoongozwa na kiti kinachopendelea CCM taifa linaongozwa na kundi la watu linalokaa Dar es Salaam linaloamua juu ya Watanzania wote kwenye matumizi ya rasilimali na kusimamia sheria.
Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai alitaja sakata la gesi ya Mtwara na kusema hao ndiyo wanaoamua juu ya rasilimali za nchi wala si madiwani, wabunge, watendaji kata ama wenye viti wa CCM.
Alihoji ni kwanini waziri mmoja asimamie sekta ya nishati, gesi, uranium, tanzanite, na anafanya maamuzi peke yake na kutaka kuwe na utatuzi?
Alisema Chadema haikubaliani na mtu mmoja kufanya maamuzi ya nchi nzima peke na pia akauponda utaratibu wa sasa wa uongozi wa kuteuliwa kusimamia rasimali za nchi badala ya ule wa kuchaguliwa na Watanzania.    
KATIBA
Alisema Chadema haiko tayari kushiriki mchakato wa kutengeneza katiba mbovu na kwamba wanachotaka ni kuwa na katiba itakayoponya majeraha, kuondoa makovu ya migogoro na kuleta suluhu baina ya watu.
Alisisitiza kuwa hawatakubaliana na mchakato usio wa kisheria na ikibidi watakwenda mahakamani kwani katiba wanayotaka ni ya taifa na si ya CCM, kabila au  kundi ful
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment