Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwaipopo, alipotembelewa na ujumbe wa Chama cha Conservative cha nchini Uingereza, ili kujifunza jinsi CHADEMA inavyofanya kazi za siasa hususan katika kuisaidia jamii.
Alisema katika vyama 19 vya siasa nchini, ambavyo vinazungumzia kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye makucha ya walanguzi na ufisadi ni CHADEMA pekee chenye sera hiyo, kutokana Watanzania kugundua hilo ndipo wakaamua kukiunga mkono.
“Chimbuko la mafanikio ya chama chetu ni kutokana na jinsi tulivyojipanga katika kupigania haki na kuhakikisha tunasimamia maslahi ya umma wa Watanzania,” alisema Mwaipopo.
Awali ujumbe huo ulitaka kujua njia walizopita CHADEMA hadi kupata mafanikio hayo ya haraka kuliko vyama vingine nchini.
Kate Fulle, Mkufunzi wa Elimu ya kampeni na uchaguzi wa chama hicho cha Conservative, alisema chama chao kilianza kama CHADEMA kwa kupigania sera zake hususan kuelimisha umma kuhusu kusimamia haki zao na maslahi yao kitendo kilichofanya wananchi wakichague na kuongoza nchi.
“Nawapongeza sana kwani mmeweza kwenda kasi ya haraka kuliko hata sisi wakati tulipoanza na anaamini mafanikio hayo ni ya kujivunia kwa kila mpigania haki na maslahi ya umma,” alisema Fulle.
Fulle alisema kutokana na mafanikio hayo, ni matarajio ya chama chake kuwa CHADEMA katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015 itapata mafanikio zaidi ukilinganisha na awali.
Ujumbe huo wa watu wawili ambao ni Kate Fulle na Duncan, unatarajiwa kuondoka nchini Aprili 21 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment