Wakati wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakipanga kufanya maandamano makubwa leo jijini Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya kushinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ajiuzulu, Jeshi la Polisi limewapiga marufuku kwa maelezo kuwa maandamano hayo ni batili.
Takriban wiki mbili zilizopita viongozi wa chama hicho katika mikoa hiyo, kwa nyakati tofauti walitangaza kufanyika kwa maandamano hayo, lengo likiwa ni kushinikiza Dk Kawambwa na naibu wake, Philipo Mulugo kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana.
Wakati polisi wakizuia maandamano hayo kwa maelezo kuwa Serikali imeshaunda tume inayoongozwa na Profesa Sifuni Mchome, kuchunguza chanzo cha kufeli kwa asilimia 65 kwa watahiniwa hao, Chadema wamesema lazima maandamano yafanyike na wako tayari kufa.
Kauli ya Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesisitiza kuwa maandamano ya kumshinikiza Dk Kawambwa kujiuzulu yatafanyika kesho kama yalivyopangwa licha ya Jeshi la Polisi kuyapiga marufuku.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesisitiza kuwa maandamano ya kumshinikiza Dk Kawambwa kujiuzulu yatafanyika kesho kama yalivyopangwa licha ya Jeshi la Polisi kuyapiga marufuku.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mbowe alisema iwapo Serikali itaamua kutumia risasi na mabomu kuua raia wake wanaoandamana kwa amani kuonyesha hisia ya kuchukizwa na matokeo mabaya ya kidato cha nne, basi itimize dhamira hiyo kwa kuwapiga risasi waandamanaji.
“Kama CCM na serikali yake itatumia risasi na mabomu kuua watu kumlinda waziri mmoja asijiuzulu, basi wafanye hivyo. Sisi tutaandamana kama tulivyotangaza mwezi mmoja uliopita na tunaomba dunia ielewe hivyo,” alisema Mbowe.
Alisema wameamua kuendelea na maandamano hayo baada ya kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na polisi kuzuia maandamano hayo, ikiwamo ile ya CCM kudaiwa kuandaa maandamano siku hiyohiyo kupitia njia zilezile zilizotajwa na Chadema.
Mbowe alisema maandamano hayo yatafanyika katika majiji manne ya Arusha, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam na kuwataka wananchi wanaoishi jirani na miji hiyo kujitokeza kwa wingi kuandamana kwa mustakabali wa watoto wao wasiopata elimu bora kama wapatayo wale wa viongozi.
Chadema Mkoa wa Dar
Katibu wa Chadema Kanda ya Dar es Salaam, Henry Chilewo akizungumza na vyombo vya habari jana alisema, maandamano hayo yatahusisha wananchi wa kada zote.
“Mwenyekiti wetu (Freeman Mbowe) alitoa siku 14 kwa viongozi hao wajiuzulu kwa hiyari lakini wamegoma, tunaamini nguvu ya umma wa Watanzania itafanikisha hilo na ifahamike wazi kuwa lengo letu ni kudai elimu bora kwa watoto wetu,” alieleza Chilewo.

Kauli ya Kamanda Kova
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliliambia gazeti hili kwamba bado jeshi hilo linafanya tathmini kabla ya kutoa kauli ya mwisho.
“Bado tunafanya tathmini, kesho (leo) tutaeleza kama yatakuwapo au hayatakuwapo,” alisema Kova.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, Englebert Kiondo alisema maandamano hayo ni batili kwa sababu tume imeshaundwa.
“Kesho (leo) Rais wa China, Xi Jingping anakuja nchini hivyo si vizuri akafika na kukutana na maandamano, nawaomba wananchi wa Temeke wasishiriki katika maandamano haya, waendelee na shughuli nyingine,” alisema Kiondo.
Katika ufafanuzi wake, Chilewo alisema, “Polisi wanapewa taarifa tu siyo maombi, wakubali wakatae sisi lazima tuandamane, hatuwezi kusitisha maandamano kwa sababu ya ujio wa Rais wa China.”
Alisema maandamano katika wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke yataanza saa 3:00 asubuhi kwenye ofisi za jimbo la Kinondoni, kwamba maandamano yataanzia katika ofisi za chama hicho katika wilaya hizo, kuelekea katika viwanja vya Jangwani.
“Waandamanaji wote wakifika Jangwani wataanza safari kuelekea Ofisi za Waziri Mkuu,” alisema Chilewo.
“Waandamanaji wote wakifika Jangwani wataanza safari kuelekea Ofisi za Waziri Mkuu,” alisema Chilewo.
Mkoani Mbeya
Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo pamoja na Muungano wa Chama cha Machifu (Mujata) imepiga marufuku maandamano hayo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo pamoja na Muungano wa Chama cha Machifu (Mujata) imepiga marufuku maandamano hayo.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Norman Sigalla ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya alisema kuwa kamati hiyo imeona hakuna sababu za msingi za chama hicho kufanya maandamano hayo kwani tayari Waziri Mkuu ameshaunda tume ya kuchunguza sababu za kuwapo matokeo mabaya ya kidato cha nne.
“Tunafahamu wote matokeo ya kidato cha nne hayakutufurahisha, lakini tayari Waziri Mkuu ameunda tume sasa kufanya maandamano ni kutaka kuvunja amani katika mkoa wetu na kwa nini yafanyike hapa Mbeya na wasifanyie kwao?” Alihoji na kuongeza;
“Wanaotaka kuandamana hapa siyo kwao bali wanachotaka ni kuwaingiza matatani watoto wetu ambao hawana hatia wapigwe virungu, hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama imeamua kuwa haitavumilia kuona maandamano hayo yanafanyika hapa Mkoani kwetu,” alisema.
Jijini Mwanza
Jeshi la polisi limewaonya viongozi wa Chadema mkoani humo kutofanya maandamano ya kushinikiza kujiuzulu kwa waziri huyo, ambayo yalipangwa kufanyika kesho.
Jeshi la polisi limewaonya viongozi wa Chadema mkoani humo kutofanya maandamano ya kushinikiza kujiuzulu kwa waziri huyo, ambayo yalipangwa kufanyika kesho.
Kauli hiyo ya polisi inakuja wiki moja baada ya Katibu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Robert Renatus kufanya mkutano katika Hoteli ya Gold Crest na kutangaza kuwa lazima maandamano hayo yatafanyika kesho.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Magu alisema, “Tunazuia maandamano kwa sababu inaweza kuzuka vurugu, mara nyingi maandamano yanayofanywa na chama hiki huibuka vurugu na kuingilia shughuli za watu.”
Alifafanua kuwa tayari Serikali imeshaunda tume kwa ajili ya kufuatilia matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne, hivyo maandamano hayo hayatakuwa na manufaa yoyote, huku akiwaonya wafuasi wa chama hicho kutofanya maandamano kwa kuwa hawajapewa kibali na jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment