Leo kumefanyika Mkutano mkubwa Mjini Igunga uliohutubiwa na viongozi wakuu wa CHADEMA Wilaya pamoja na Viongozi wengine wa Chadema makao makuu Benson Kigaila na Waitara.
Mambo muhimu yaliyozungumziwa ni pamoja na yafuatayo
Wananchi wametakiwa kuwa na umoja juu ya kutetea maslahi yao ambayo imeonekana kabisa CCM imeshindwa kuyatekeleza, hivyo wametakiwa kuiunga mkono CDM kwani kwa sasa hakuna tena Chama cha upinzani nchini zaidi ya CDM nah ii inajidhihirisha wazi kwani kwa sasa adui mkubwa wa CCM ni CHADEMA na sio maladhi, umasikini na elimu duni kwa watanzania.
Pia wananchi wamepewa taarifa juu ya Kukamatwa kwa Lwakatare na wananchi wameelezwa juu ya hila za CCM na hali halisi ya jinsi alivyokamatwa na tuhuma zilizopikwa na CCM na serikali yake na kwa msisitizo viongozi hawa wamewataka wananchi kupuuzia Propaganda za CCM ambazo kila kukicha wanaziandaa ili kutaka kuidhoofisha CDM na mwisho wa siku uumbuka.
Pia suala la maji kwa wananchi wa Igunga lilizungumziwa kwa wananchi kuelezwa juu ya Ufisadi uliofanyika ambapo katika Ziara ya Rais Kikwete alizindua Mradi wa maji ambao uliitwa Mradi Mkubwa wa Maji Igunga lakini cha kustaajabisha Baada ya kuanza kutumika imeonekana chujio lililojengwa na dogo na halitoshelezi mahitaji na kufanya huduma za maji mjini igunga kudhorota kiasi idara ya maji imeanza kufungulia njia nyingine inayoleta maji taka mjini sasa wananchi wameulizwa tulikuwa tunatoka Analog kwenda Digital leo tunarudishwa tena analog tunatakiwa tuwe na kauli moja ya kukataa udhalimu na wizi huu ambao unafanyika kwa kutokuwa na usimamizi madhubuti wa hii serikali ya CCM kwani viongozi wa Juu wanapokwapua fedha za serikali na hawa wa chini nao wanafanya vivyo hovyo na mwiso wa siku wanaumia wananchi wote.
No comments:
Post a Comment