Baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi ya kukusanya maoni ya wananchi sasa inaanza kuyachambua na kuandika Rasimu ya Katiba Mpya, huku ikitoa utaratibu wa kupatikana mabaraza ya katiba ya kata.
Kazi ya kukusanya maoni hayo iliwahusisha wananchi mmoja mmoja kupitia mikutano na ilikamilishwa na Tume DesBaadaye Tume ilikutana na makundi maalum na watu mashuhuri, wakiwamo viongozi wastaafu na waliopo madarakani, Januari 7-28, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, aliwaambia waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana kuwa, baada ya kukamilisha kazi hiyo, hatua inayofuata ni uchambuzi wa maoni yote yaliyokusanywa na uandishi wa Rasimu ya Katiba.
Alisema rasimu hiyo itawasilishwa katika mikutano ya mabaraza ya katiba ya kata itakayofanyika kuanzia Juni, mwaka huu.
“Kama nilivyosema hapo awali, Tume imemaliza kazi ya kukusanya maoni binafsi ya wananchi na pia imemaliza kazi ya kukutana na makundi maalum na hivyo kukamilisha kazi ya ukusanyaji maoni,” alisema Jaji Warioba.
Alisema katika mikutano na makundi, Tume ilikutana na vyama vya siasa 19; taasisi za kidini 22; asasi za kiraia 72; taasisi za kiserikali 71 na viongozi na watu mashuhuri 43 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, Rasimu ya Katiba Mpya itakayoandaliwa itachapishwa katika magazeti mbalimbali kama Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 inavyoelekeza.
Alisema hatua hiyo itachukuliwa ili wananchi wapate fursa ya kuisoma kabla ya rasimu hiyo kuwasilishwa rasmi katika mabaraza ya katiba ya kata yatakayoitishwa na Tume nchini kote.
Jaji Warioba alisema mikutano ya mabaraza ya katiba itafanyika Juni, mwaka huu na itajumuisha wajumbe watakaochaguliwa na wananchi wenyewe, kuanzia ngazi ya kijiji.
Alisema wajumbe hao watapaswa kuwakilisha maoni ya wananchi katika mikutano ya mabaraza.
Jaji Warioba alisema kwa sasa Tume imekamilisha mwongozo wa namna bora na ya kidemokrasia ya kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya kata.
Alisema mwongozo huo utasambazwa nchini kote na kwamba, tayari umeanza kutangazwa katika vyombo vya habari ili wananchi waufahamu na kuutolea maoni ya kuuboresha.
MABARAZA YA KATIBA TANZANIA BARA
Jaji Warioba alisema kwa mujibu wa mwongozo huo, katika mikoa ya Tanzania Bara ukiondoa Dar es Salaam, kila kata itawakilishwa na wajumbe wanne watakaoungana na madiwani wa kata na viti maalum katika Baraza la Katiba la Wilaya.
Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Tume imeandaa utaratibu tofauti wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya.
Katika utaratibu huo, alisema kila kata watatoka wajumbe wanane watakaoungana na madiwani wa kata na viti maalum.
“Kwa msingi huo, kutakuwa na jumla ya wajumbe 18,169 watakaohudhuria mabaraza ya katiba ya wilaya kwa Tanzania Bara,” alisema Jaji Warioba.
MABARAZA YA KATIBA ZANZIBAR
Jaji Warioba alisema kwa upande wa Zanzibar, kutakuwa na mabaraza ya katiba ya wilaya ngazi ya mamlaka ya serikali za mitaa 13.
Alisema kila shehia visiwani humo itawakilishwa na wajumbe watatu watakaoungana na madiwani wa wadi, viti maalum na wale wa kuteuliwa waliopo kazini kwa sasa.
“Kwa msingi huo, wajumbe wote wa mabaraza ya katiba kwa Zanzibar watakuwa 1,198,” alisema Jaji Warioba.
SIFA ZA WAJUMBE WA MABARAZA
Jaji Warioba alisema muombaji wa ujumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya anatakiwa awe raia wa Tanzania; awe na umri wa miaka 18 au zaidi; na awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
Alisema pia anatakiwa awe mkazi wa kudumu wa kijiji/mtaa/shehia husika; awe mtu mwenye hekima, busara na uadilifu; na awe mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo.
WITO KWA WANANCHI
Jaji Warioba aliwataka wananchi wanaopenda kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya kuwasilisha majina yao kwa maofisa watendaji wa vijiji/mitaa kwa Tanzania Bara.
Kwa upande wa Zanzibar, alisema wanatakiwa kuwasilisha kwa sheha katika tarehe itakayoelekezwa na Tume hapo baadaye.
Alisema mara watakapopatikana, wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya watakuwa na jukumu la kujadili Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Tume kabla ya rasimu hiyo kuwasilishwa katika Bunge Maalum la Katiba ili kujadiliwa.
Hata hivyo, alisema mikutano ya mabaraza ya katiba itakayofanyika nchini kote kuanzia Juni, mwaka huu, haitahusu kupiga kura. Alisema mikutano hiyo itakuwa ya kujadili Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Tume na kutoa maoni ya kuiboresha.
Aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kuwapata wajumbe watakaoshiriki katika mabaraza kwa mujibu wa mwongozo, ambao Tume imeutangaza kupitia vyombo vya habari na kusambazwa katika wilaya zote.emba 19, mwaka jana

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment