Wednesday, December 5, 2012

Mnyika kuwasilisha hoja binafsi Halmashari ya Jiji


MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), anatarjia kuwasilisha hoja binafsi leo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, inayohusu uboresha wa upatikanaji huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika maeneo mbalimbali jijini.
Akizungumza na wandishi wa habari kwa niaba ya mbunge huyo, jijini Dar es Salam jana, Katibu wa Mbunge huyo, Aziz Himbuka, alisema lengo la hoja hiyo ni kupendekeza baraza la madiwani wa jiji kujadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka zaidi za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa maji taka katika jimbo la Ubungo na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla.
Alisema mbunge huyo ameamua kuchukua hatua hiyo, ili Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iweze kutimiza wajibu wake mwezi huu, huku akisubiri kuwasilisha hoja binafsi bungeni katika mkutano wa 10, Februari mwakani endapo Wizara ya Maji haitachukua hatua zinazostahili.
Himbuka alisema pamoja na mafanikio ya kawaida yaliyopatikana kupitia mikutano yake na wananchi katika kata mbalimbali jimboni na ufuatiliaji serikalini, bado yapo matatizo yanayohitaji baraza la madiwani kushughulikia.
Alisema katika kufuatilia masuala ya maji, Mnyika alianza kwa kufanya kongamano la maji katika jimbo la Ubungo mwanzoni mwa mwaka 2011, ili kuwakutanisha wananchi, mamlaka husika na wadau wengine katika kuunganisha nguvu kupata ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment