Mh. Vincent Nyerere apokelewa kama mfalme Iringa
Mh. Vincent Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini ametua katika Manispaa ya Iringa na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa mji huo kama mfalme. Mapokezi hayo makubwa yamesababisha watu kuacha shughuli zao na kufurika katika uwanja wa Mwembe Togwa kumsikiliza Mbunge huyo ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mheshimiwa Nyerere amepokelewa na Mwenyeji wake Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini. Sasa hivi Mh. Nyerere ndio anakaribishwa kuhutubia maelfu wa wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwembe Togwa.
No comments:
Post a Comment