
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anaanza ziara ya siku tatu wilayani Karatu ambako pamoja na mambo mengine, atakutana na viongozi wa wilaya na madiwani wa chama hicho kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Katibu wa Chadema mkoani Arusha, Amani Golugwa, alithibitisha habari kuhusu ziara hiyo.
“Ni kweli kwamba mwenyekiti atafanya ziara wilayani Karatu na lengo la ziara hiyo ni kuimarisha chama, kazi ambayo ni moja ya majukumu ya viongozi wote. Atakutana na kamati ya utendaji ya chama wilayani Karatu pamoja na madiwani wote wa Chadema,” alisema Golugwa
“Ni kweli kwamba mwenyekiti atafanya ziara wilayani Karatu na lengo la ziara hiyo ni kuimarisha chama, kazi ambayo ni moja ya majukumu ya viongozi wote. Atakutana na kamati ya utendaji ya chama wilayani Karatu pamoja na madiwani wote wa Chadema,” alisema Golugwa
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Golugwa alisema Mbowe atakayeongozana na viongozi wa chama hicho mkoani Arusha, pia atatumia ziara hiyo kutafuta ufumbuzi wa mpasuko unaodaiwa kukikumba chama hicho wilayani Karatu.
Kamati Kuu ya Chadema (CC), iliyokutana jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ilitangaza kuusimamisha kwa muda, uongozi wa chama hicho wilayani Karatu, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili baadhi ya viongozi.
Ingawa wengi wamekuwa wakidai kuwa mgogoro huo unachchoewa na harakati za kisiasa, hasa za ubunge 2015, lakini uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa tatizo mo uongozi usioridhisha katika halmashauri ya Karatu inayoongozwa na Chadema.
Wakati mradi wa maji Karatu ndiyo unaotajwa kusababisha mgogoro, suala kubwa linalowakera wananchi wilayani humo kiasi cha kutishia uhai wa Chadema kilichoongoza jimbo la Karatu kwa zaidi ya miaka 17 sasa ni ugawaji holela wa ardhi kwa wawekezaji wa ndani nan je unaofanywa na uongozi wa halmashauri hiyo bila kujali maslahi ya umma.
Chadema pia inaongoza Halmashauri ya Wilaya ya Karatu tangu mwaka 2,000 hadi sasa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani kulinganisha na CCM.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment