Chama cha Mapinduzi CCM kiko katika hali mbaya katika Jimbo la Kwimba baada ya maelfu ya wanachama wake pamoja na viongozi kadhaa kuhamia CHADEMA.CHADEMA imezoa wanachama 15000 katika mikutano mikubwa sita iliyopigwa katika kata kadhaa za wilaya hiyo.
Mikutano hiyo ilihutubiwa na kiongozi mkuu wa M4C Kanda ya Ziwa Alphonce Mawazo.Kiongozi huyo alisema wananchi wameamua kuhama kutoka kwenye siasa za CCM za Analogia na kuhamia siasa za CHADEMA za Digitali.
Wachunguzi wa kisiasa wilayani Kwimba wanasema CCM ina hali mbaya wilayani humo na kuna uwezekano mkubwa uchaguzi ujao CHADEMA kuzoa ubunge na madiwani wote wilayani humo.
Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment