Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepinga maagizo yaliyotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwataka watumishi wa umma kuhudhuria mikutano ya CCM na kutoa taarifa za kiserikali.
Kadhalika, chama hicho kimemshauri Rais Jakaya Kikwete, kukemea kauli kama hizo kwani ni kinyume cha haki za kikatiba, misingi ya utawala bora, sheria na waraka wa utumishi wa umma.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kwamba maagizo hayo ni ishara ya udhaifu na uzembe unaosababishwa na operesheni ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chadema.
“Maagizo haya ya CCM yanaashiria udhaifu wa chama hicho wa kuzidiwa na vuguvugu la mabadiliko na madai ya uwajibikaji toka kwa umma kwa kiwango cha kutaka kuirejesha nchi katika maagizo ya mfumo wa siasa wa chama kimoja kwamba kundi lote la watumishi wa serikali na vyombo vyake walikuwa wakilazimishwa kushiriki katika shughuli za CCM,” alisema Mnyika.
Alisema jambo hilo kwa sasa haliwezekani kwa kuwa watumishi wengine ni wanachama wa Chadema na wapo ambao sio wanachama wa chama chochote cha siasa.
Alikumbusha mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali ya mwaka 1991 na marekebisho ya Katiba ya mwaka 1992 kuingia katika mfumo wa vyama vingi na marekebisho ya sheria mbalimbali, kuwa yaliweka uhuru wa watumishi wa umma kujiunga na vyama vya siasa (isipokuwa watumishi wa kada maalum) na mipaka ya mahusiano kati ya kazi zao za kiserikali na shughuli za vyama vya siasa kikiwemo chama kinachotawala.
“Naitaka CCM izingatie kuwa utumishi wa umma katika nchi yetu unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake” alisema na kuongeza:
"Waraka wa utumishi wa umma wa mwaka 2000 unawataka kutekeleza wajibu wao wa utumishi bila kufanya upendeleo wala ubaguzi wa chama chochote cha siasa.”
Alisema waraka huo unawakataza watumishi wa umma kuzungumza na kutoa taarifa kwenye mikutano ya vyama vya siasa na haujatoa ruhusa kwa watumishi hao kuzungumza katika mikutano ya CCM pekee; hivyo maagizo yaliyotolewa na chama hicho ni kinyume na maagizo ya serikali inayoongozwa na chama hicho.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment