Monday, October 29, 2012

Tafsiri na uchambuzi wa matokeo ya udiwani- Dr Kitila Mkumbo

Hadi dakika hii matokeo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, CHADEMA wameshinda katika kata 5 and TLP (1) na CCM kushinda katika kata zilizobaki. 

Kwa muono wa karibu unaweza ukadhani kwamba CHADEMA wamepoteza sana katika uchaguzi huu. Hata hivyo ukiyachunguza matokeo haya kwa ukaribu utaona kwamba CHADEMA wamepata mafanikio makubwa na CCM wametelemka. 

Tukumbuke kwamba CHADEMA walikuwa na kata mbili za kuzilinda katika uchaguzi huu ambazo ni Rombo na Mvomero. Kata hizi wamefanikiwa kuzilinda na kuongeza zingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole na Daraja Mbili (zote hizi zilikuwa za CCM). Kwa hiyo wamelinda kata zao na kuzipokonya zingine tatu kutoka mikononi mwa CCM. 

Na yote hii ni ndani ya miezi 24 tu tangu uchaguzi mkuu ufanyike. Kwa hiyo kimehesabu CCM wameshuka kwa 11.1% na CHADEMA wamepanda kwa 60%! So, CDM keep up the momentum!


Chanzo - JF

No comments:

Post a Comment